The House of Favourite Newspapers

Uchumi yafunga maduka yake Tanzania na Uganda

0

Uchumi Supermarket  lililopo Makumbusho. 

MADUKA ya jumla ya Uchumi yametangaza kufungwa shughuli zake nchini Tanzania na Uganda katika zoezi la kubana matumizi .

Mkurugenzi mkuu wa maduka hayo Dr. Julius Kipng’etich, amesema  bodi yake imeamua kufunga maduka hayo kwa lengo la kutathmini muundo wa shughuli zake nchini Kenya. ”Maduka yetu nchini Tanzania na Uganda yanafanyiza asilimia 4.75 ya oparesheni zetu licha ya kutugharimu asilimia 25 ya shughuli zote,” alisema mkurugenzi huyo.

Maduka ya uchumi katika mataifa hayo mawili hayajazalisha faida yoyote katika kipindi cha miaka mitano jambo ambalo linalazimisha faida zinazopatikana katika maduka ya Kenya kutumika katika maduka hayo,alisema Kipng’etich.

Mkurugenzi huyo amesema kuwa tayari maduka hayo yameandika barua kwa Mamlaka ya Masoko nchini Kenya na kwenye Soko la Hisa na wadau muhimu kuhusu uamuzi huo na kuongezea kwamba hivi karibuni kampuni hiyo itahitaji kuungwa mkono na wamiliki wa hisa ili kuidhinisha mpango huo.

Maduka yote katika mataifa hayo mawili yamefungwa.

Leave A Reply