The House of Favourite Newspapers

Uefa Champions League Kutimua Vumbi leo

0

 

PAZIA rasmi la Ligi ya Mabingwa Ulaya (UEFA Champions League) linafunguliwa leo kwenye hatua ya makundi ambapo mechi kadhaa zitachezwa, lakini macho na matarajio ya wengi yatakuwa katika Jiji la raha Paris nchini Ufaransa wakati mabingwa wa Ligue 1 Paris Saint Germain PSG watawakaribisha Mashetani Wekundu wa Old Trafford, Manchester United.

 

United wanaingia kwenye mchezo huo wakiwakosa nyota wao kadhaa akiwemo nahodha Harry Maguire ambaye aliumia kwenye mechi ya ligi kuu dhidi ya Newcastle, na usajili wao mpya, Edison Cavan, hajasafiri na timu pamoja na kinda Mason Greenwood.

 

Meneja wa Manchester United amethibitisha nyota wake, Bruno Fernandes, kuwa ndiye atakayekuwa nahodha kuwaongoza wenzake kuwakabilii vijana wa Tuchel.

Neymar huenda akawa yupo vizuri kucheza leo baada ya kupumzishwa kwenye mechi ya ligi, Draxler na Marquinhos, wanatarajiwa kurudi baada ya kupona majeraha na Leandro Paredes na Marco Verratti watakaokosa mchezo kwa sababu ya majeruhi.

 

Chelsea watakuwa darajani Stamford Bridge na kibarua kizito kuwakabili mabingwa wa Uropa Sevilla  kutoka nchini Uhispania, The Blues, hawajaanza vizuri sana ligi kuu EPL safu yake ya ulinzi inaruhusu magoli mengi.

 

Kurejea kwa Hakim Ziyech na Pulisic kutaipa nguvu ikiwa ni pamoja na Thiago Silva, Kipa Edouard Mendy watakosekana kwenye mechi hiyo.

 

Mechi nyingine zitakuwa ni Dynamo dhidi ya Juventus, Barcelona watacheza na Ferencvaros, Lazio dhidi ya Borossia Dortumnd, RB Leipzeg watavaana na Instambul Buyuksehir.

 

 

Leave A Reply