Ufaransa Yaichapa Ubelgiji, Yatinga Fainali Kombe la Dunia – Video

Timu ya taifa ya Ufaransa imefanikiwa kutinga hatua ya fainali ya michuano ya kombe la Dunia baada ya kuifunga Ubelgiji bao 1 – 0, bao ambalo lilifungwa dakika ya 51 na mlinzi, Samuel Umtiti.

 

Mchezo wa pili wa nusu fainali unatarajiwa kupigwa hapo kesho baina ya timu ya taifa ya Uingereza dhidi ya Croatia ambapo mshindi wa mechi hiyo atakabiliana na Ufaransa tarehe 15 siku ya Jumapili.

Hii ilikuwa nusu fainali ya pili kwa Ubelgiji wakiwa na kumbukumbu ya kucheza mara moja na kupoteza dhidi ya Argentina mwaka 1986.

 

Ufaransa imefanikiwa kutinga fainali kwa mara ya tatu ndani ya miaka 20. Mwaka 1998 ambapo walitwaa kombe wakiwafunga Brazil kwenye mechi ya fainali na 2006 ambapo walifungwa na Italia na 2018 baada ya jana kushinda bao 1-0 dhidi ya Ubelgiji.

 

Highlights 2018 FIFA World Cup Semi-Final 1: France vs Belgium

Loading...


Stori zinazo husiana na ulizosoma

Toa comment