The House of Favourite Newspapers

Uhangaika Kutafuta Bando Kubwa la Bei Nafuu? Soma Hapa

phoneUKISIKIA nyumbani kumenoga, maana yake kumenoga kweli, fanya urudi fasta! Unaambiwa kampuni mama ya simu nchini TTCL, imetambulisha mchongo mpya na wa kijanja kwa watumiaji wote wa simu janja (smartphones) ambapo sasa, unajipatia MB kibao, dakika za kupiga mitandao yote na SMS kama zote kwa bei poa kabisa!

 

Unachotakiwa kufanya, kama bado huna laini ya TTCL, wahi kwenye vituo vya huduma kwa wateja vilivyosambaa kila kona, nenda kasajili laini yako na baada ya hapo, ndani ya muda mfupi tu laini yako itasajiliwa rasmi na utaanza kufurahia huduma zote zikiwemo za kupiga na kupokea simu na kubwa zaidi, utapata huduma ya T-Pesa kwenye simu yako, ambayo itakuwezesha kutuma na kutoa fedha kwa ufanisi mkubwa kuliko mitandao mingine yote.

 

Ukishakuwa na uwezo wa kutumia T- Pesa sasa, hapo ndipo unapoweza kuanza kufurahia bando tamtam la T- Pesa. Ni rahisi sana kuweka fedha kwenye laini yako ya simu kupitia T- Pesa! Unachotakiwa kufanya, nenda kwenye kituo cha kutolea huduma au mabanda ya TTCL yaliyopo kila sehemu, mwambie mhudumu kiasi unachotaka kuweka, toa fedha zako na mkabidhi.

 

Muda mfupi baadaye, utapokea ujumbe unaoonesha kiasi cha fedha kilichoingizwa kwenye akaunti yako.

 

Baada ya kuhakikisha akaunti yako ina fedha, sasa utatakiwa kupiga namba *150*71# kisha utachagua kifurushi cha Bando Tamtam kinachokufaa. Kwa shilingi 500/= tu, utapata intaneti MB 500, dakika 5 za kupiga mitandao yote na SMS 50 kwa muda wa saa 24.

 

Kwa shilingi 1000/=, utapata bando la wiki ambalo ndani yake kutakuwa na intaneti GB 1, dakika 5 za kupiga mtandao wowote na SMS 100 na bando lako litadumu kwa muda wa siku saba.

 

Ukitaka kujiunga bando la mwezi, kwa shilingi 5000/= tu utapata intaneti GB 2, dakika 20 za kupiga mitandao yote, SMS 300 kwa muda wa siku 30! Unangoja nini? TTCL wanakwambia rudi nyumbani kumenoga.

 

Uzuri zaidi ni kwamba intaneti ya TTCL, ina kasi ya ajabu ambayo itakuwezesha kuperuzi kwenye mitandao ya kijamii kama Facebook, Instagram, WhatsApp, Telegram na mingine kibao kwa urahisi zaidi.

 

Kwa wale wapenzi wa kutazama video YouTube, pia TTCL ndiyo jibu lao kwa sababu intaneti inayotolewa, inamuwezesha mteja kutazama video kwa ufanisi wa hali ya juu, hakuna kukwamakwama (buffering) wala intaneti kuyumba.

 

Bando Tamtam la T- Pesa, ni sehemu ndogo tu ya mambo mazuri yanayopatikana kutoka TTCL, vipo vifurushi vingine kibao vikiwemo T-Connect vinavyompa mteja huduma ya intaneti ya 4G, Jiachie, Nyumbani Pack, Nduki Pack na kadhalika.

 

Kwa maelezo zaidi, unaweza kupiga simu kwa namba 100 kupitia laini yako ya TTCL ambapo utapewa maelekezo yote muhimu na wahudumu wachangamfu. Lakini pia unaweza kutembelea website ya TTCL kwa kubofya www.ttcl.co.tz au unaweza kuwatembelea kwenye page zao za mitandao ya kijamii Twitter: TTCLCorporation na Facebook: TTCLTanzania.

Rudi nyumbani, kumenoga!

Makala: MWANDISHI WETU, DAR

 

Comments are closed.