The House of Favourite Newspapers

Uingereza Yaridhishwa Mchakato wa Uchaguzi TZ

0

NCHI  ya Uingereza imesema inaridhishwa na namna mchakato wa uchaguzi unavyoendelea hapa nchini.

 

Hayo yamebainishwa leo Oktoba 5, 2020, na Balozi wa Uingereza hapa nchini David Concar mara baada ya kukabidhi hati ya utambulisho kwa Rais John  Magufuli,  Ikulu jijini Dar es Salaam.

 

Amesema kuwa nchi ya Uingereza ni mdau mkubwa katika kusaidia maendeleo ya nchi mbalimbali zinazoendelea.

 

Aidha  amebainisha kuwa atasaidiana na Rais Magufuli katika kujenga uchumi mara baada ya janga la Corona, pamoja na kuipa sifa Tanzania namna inavyopambana na ugonjwa huo.

 

Kabla ya kuja Tanzania, Concar  alihudumu kama Balozi wa Uingereza nchini Somalia toka mwaka 2016 hadi 2019.

Leave A Reply