The House of Favourite Newspapers

Serikali Yakanusha Mtaala Cheti cha Ualimu Awali, Msingi Kufutwa

0

 

SERIKALI Imekanusha taarifa zilizosambaa kuwa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imefuta mtaala wa ualimu wa ngazi ya cheti kwa elimu ya awali na msingi ikiwa ni hatua ya kuboresha elimu nchini.

 

Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Gerson msigwa amesema taarifa hiyo si ya kweli na ipuuzwe.

 

……………Taarifa hiyo ilisema kuwa…………..

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imefuta mtaala wa ualimu wa ngazi ya cheti kwa elimu ya awali na msingi ikiwa ni hatua ya kuboresha elimu nchini.

 

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo, Naibu Katibu Mkuu wizara hiyo, Dkt Ave Maria Semakafu, amesema hatua hiyo inakwenda sambamba na kufanyia  kazi maoni ya wadau ambao wamekuwa wakiyatoa likiwemo kufuta mtaala huo.

 

“Mtaala ulioboreshwa unatoa nafasi kwa mwalimu katika mwaka wa pili wa masomo kuchagua eneo la umahiri atakalobobea tofauti na mfumo wa zamani ambao haukuwa katika muktadha huo,” amesema.

 

Amesema mtaala huo mpya utaanza kutumika katika mwaka wa masomo 2020/2012  na kwamba mwalimu yeyote mwenye cheti cha ualimu atakuwa na sifa ya kusomea Diploma ya Ualimu wa Elimu ya Awali au Msingi na vile vile atakapohitimu na kufaulu atakuwa na sifa ya kujiunga na chuo kikuu kupata shahada ya kwanza ya ualimu kwa elimu ya awali  au msingi.

 

“Programu itakayofundishwa itakuwa ya miaka mitatu na masomo yatafundishwa kwa lugha mbili ambazo ni Kingereza na Kiswahili kutokana na kuwepo kwa shule za English Medium nchini,” amesema.

 

Amesema waliosoma Astashahada (cheti) bado serikali inatambua uhitimu wa cheti katika kada ya ualimu na ipo kwenye mfumo wa utumishi na itaendelea kuwepo na hakuna mwalimu atakayefukuzwa kazi kwa kuwa yeye ni mwalimu wa ngazi ya cheti.

 

Kwa mujibu wa Semakafu, walimu walioko kazini watakaopenda kujiendeleza wanaweza kusoma kwa masafa kupitia Taasisi ya Elimu Tanzania  (TIE) kwa njia ya masafa, njia ambayo haitaathiri utendaji  na mwisho kufanya mitihani ili kupata Stashahada.

 

“Kwa walimu ambao wana vyeti na hawajaweza kupata fursa ya ajira, watatakiwa kurudi vyuoni na kuweza kupata Diploma ya Ualimu,” amesema.

Leave A Reply