The House of Favourite Newspapers

Uingereza Yatuma Mtambo wa Makombora ya Roketi Nchini Ukraine

0
M270 Multiple Launch Rocket Systems.

NCHI ya Uingereza kwa mara ya kwanza imepuuza vitisho vya Rais wa Urusi Vladimir Putin na kuamua kutuma mtambo maalum na wa kisasa wa kufyatua makombora ya roketi unaofahamika kama

 

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi ya Uingereza Ben Wallace amesema mtambo huo utaisadia nchi ya Ukraine kujihami na kujilinda dhidi ya uvamizi wa Urusi.

 

Serikali ya Uingereza bado haijathibitisha ni zana ngapi zitapelekwa nchini Ukraine lakini kwa mujibu wa Shirika la Utangazaji la Taifa, BBC limebainisha kuwa ni jumla ya mitambo mitatu inayotumwa kwa hatua ya mwanzo kabisa.

 

Mpango huo wa kupelekea mitambo ya kurusha makombora ya roketi ulianza kuasisiwa na Serikali ya Marekani ambapo wiki iliyopita ilituma mitambo hiyo, kitendo ambacho kilikemewa mara moja na Serikali ya Moscow huku Rais Putin akitoa tahadhari kuwa ataanza kulenga maeneo mapya hasa ya wale wanaoisaidia Ukraine kwa zana za kivita.

Ben Wallace Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi ya Uingereza

Sambamba na hilo Serikali ya Uingereza imesema wanajeshi wa Ukraine watafundishwa namna ya kutumia mitambo hiyo na mafunzo yatafanyika ndani ya nchi ya Uingereza kuanzia wiki zijazo.

 

Akiongea wakati wa kutangaza maamuzi hayo Wallace alisema Uingereza inaongoza katika kuhakikisha inasaidia vikosi vya Ukraine kupata zana na mitambo maalum kwa ajili ya kujilinda dhidi ya uvamizi wa Urusi.

 

“Kama ambavyo mbinu za Warusi zinabadilika, ndivyo ambavyo na sisi lazima tuongeze misaada yetu.”

 

Hii mitambo yenye uwezo wa kurusha makombora ya roketi kwa wingi inaweza kuwasaidia rafiki na ndugu zetu wa Ukraine kuweza kujilinda dhidi ya ukatili wa makombora ya masafa marefu ambayo Putin amekuwa akiyatumia kuteketeza miji.” Alisema Wallace

 

Mtambo huu mpya unaweza kurusha makombora ya roketi hadi umbali wa kilomita 300 na yenye uzito wa tani 25 lakini pia ndani ya dakika moja inafyatua raundi 18 za makombora ya roketi kwa kasi ya kilomita 64 kwa saa.

Leave A Reply