The House of Favourite Newspapers

Ukombozi wa Fikira; Kitabu Kinachogusa Wengi – Video

“UKIANZA kusoma ukurasa wa kwanza hadi wa mwisho hutatamani kukiweka chini. Ni kitabu kinachowainua vijana wengi na kuwasaidia katika kujiajiri na kuwa viongozi bora,” hayo ni maneno ya mwandishi mashuhuri wa hadithi, Marco Masala baada ya kuzindua kitabu chake kipya cha UKOMBOZI WA FIKRA.

 

Akizungumza na Gazeti la Ijumaa, Masala alisema, kitabu hicho kina matoleo mawili ambapo kimeandikwa kwa kutumia lugha ya Kiingereza kikiitwa LIBERATION OF THOUGHTS na kingine kwa lugha ya Kiswahili kikiitwa UKOMBOZI WA FIKRA.

 

“Kitabu hichi kilitolewa kama zawadi kwenye harusi na katika siku hiyo bibi harusi ambaye ndiye alikuwa mlengwa wa kukabidhiwa alisema no! Nakupa masharti, yaani asilimia 30 ya mauzo yake yaelekezwe kwenye kusaidia elimu ya mtoto wa kike na ndicho kinachofanyika kwa sasa.

 

“Niwaombe tu Watanzania na wapenda kusoma vitabu, kitabu hichi ni zaidi ya elimu kwani kina muundo wa hadithi, lakini ndani yake kinakupa hamasa ya kujua mafunzo mengi na watu wa rika zote,” alisema Masala na kuongeza;

 

“Uzuri wa kitabu hichi ukinunua utajua maisha halisi ya Kitanzania pili utaweza kujiajiri mwenyewe na mwisho kabisa kitakufanya uwe mfanyakazi bora kwa kukusaidia kukupa njia ya kuwasaidia walio chini nao wainuke,” alimaliza kusema Masala.

 

Ukinunua kitabu hiki utakuwa sehemu ya kusaidia elimu ya mtoto wa kike. Kama upo Dar utaletewa popote ulipo na waliopo mikoani watalipia nauli ya shilingi 8,000 au waweza kukipata kwenye maduka makubwa ya vitabu unayoyafahamu.

 

Kitabu cha Kiingereza LIBERATION OF THOUGHTS kinapatikana 20,000 wakati cha lugha ya Kiswahili, UKOMBOZI WA FIKRA kinapatikana 15,000.

Kwa mawasiliano zaidi piga namba; 0768 546 323.

Stori: MWANDISHI WETU, Ijumaa

Comments are closed.