The House of Favourite Newspapers

Harmonize Awazimia Data Mazima!

WAKATI mashabiki wakiendelea kujiuliza nini itakuwa hatima ya staa wa Bongo Fleva, Rajab Abdul ‘Harmonize’ na lebo iliyomlea kimuziki ya Wasafi Classic Baby (WCB), jamaa huyo ameamua kuzima data mazima baada ya kuonesha viashiria vya kumalizana na lebo hiyo baada ya kufuta mazima ile hashtag ya #WCB4LIFE kwenye bio ya ukurasa wake wa Instagram.

 

Wiki chache zilizopita, Harmonize au Harmo aliandika barua ya kujiondoa kwenye lebo hiyo na mmoja ya mameneja wa WCB, Sallam SK ‘Mendez’ alithibitisha kupokea barua kutoka kwa msanii huyo yenye lengo la kujitoa kwenye lebo hiyo.

 

Wiki kadhaa zilizopita, Harmo alianza kwa kufuta maneno yaliyokuwa yakimaanisha yupo chini ya lebo hiyo na kubakisha hashtag ya #WCB4LIFE lakini nayo wiki hii Harmo ameifuta kuashiria kumalizana nao kijumla.

 

Hii inaonesha ishara kuwa pengine wamefikia makubaliano ya kuacha kufanya kazi pamoja hivyo Harmo hapaswi tena kutumia nembo au neno lenye utambulisho wa lebo hiyo ya WCB au pengine kuna lingine nyuma ya pazia.

 

Alipotafutwa meneja wa Harmo, Beauty Mmary ‘Mjerumani’ ili kufafanua ishu hiyo juzi, simu yake iliita bila kupokelewa.

Comments are closed.