The House of Favourite Newspapers

Ulaji wa Mchicha Hukinga Kushambuliwa na Maradhi

KUNA utafiti uliwahi kufanywa na Chuo Kikuu cha Nottingham, unaeleza kuwa ulaji wa matunda na mboga za majani husaidia afya ya ngozi kwa njia za asili.

Hata hivyo, mboga za majani za kijani zote zina rutuba ya madini ya chuma, vitamini A na C, na zinatumika katika kupunguza uzito wa chakula, huondoa kalori na maji yaliyomo katika mboga hizo husaidia kutibu ukosefu wa choo.

 

Miongoni mwa mboga hizo ni mchicha ambao una virutubisho muhimu katika mwili wa bindamu kwa kuufanya mwili kuwa imara na kupambana na maradhi mbalimbali.

Ulaji wa mchicha kila siku utakusaidia kuzuia maradhi mbalimbali yanayoshambulia mwili. Maji ya mchicha ulioshemshwa yakitumika kila siku yanasaidia pia macho kuona vizuri huku juisi ya majani hayo yakitibu ugonjwa wa mtoto wa jicho.

Kwa mujibu wa tafiti mbalimbali za kitaalamu zilizowahi kufanyika, mchicha una faida nyingi.

 

Miongoni mwa faida hizo ni kutibu matatizo ya kuumwa mgongo, kusafisha njia ya mkojo, damu na unatibu maradhi ya figo.

Pia unatibu minyoo, baridi yabisi, tezi la shingo, homa, huongeza damu, unasaidia kupata haja ndogo kwa wingi huku ukirutubisha uwezo wa kuona vizuri.

 

Hata hivyo, umakini unahitajika katika usafishaji wa mboga za majani hasa zenye majani mengi kwa sababu zina kiwango kikubwa cha uchafu na vijidudu, iwapo hazitasafishwa vizuri.

Pia ili kupata ubora wa mboga za majani, zinapaswa zitumike vizuri katika ubora wake kwa kuoshwa vizuri kabla ya kukatwa na zipikwe zikiwa zimefunikwa na mfuniko ili zisipoteze vitamini C.

 

SALADI

Licha ya mchicha kuna watu wanapokwenda hotelini huagiza saladi tu. Salad ni mkusanyiko wa mboga za majani mabichi. Kinachotakiwa kujulikana ni kuwa ulaji wa mbogamboga zikiwa katika hali ya ubichi au zikiwa hazijapikwa una faida kubwa kiafya.

 

Hata hivyo, ulaji huo bila ya kuchukua tahadhari unaweza kusababisha magonjwa yanayoenea kutokana na kula vyakula vichafu visivyosafishwa vema. Katika maisha ya binadamu karibu kila jambo zuri linatakiwa kufanywa kwa tahadhari au kuchunga miiko yake, bila ya kufanya hivyo, faida ya jambo hilo haitapatikana na badala yake mtu anaweza kukumbwa na maradhi.

 

Ulaji wa mbogamboga zikiwa katika hali ya ubichi au zikiwa hazijapikwa una faida kubwa kiafya. Hata hivyo, ulaji huo bila ya kuchukua tahadhari utasababisha magonjwa yanayoenea kutokana na kula vyakula vichafu. Ni ukweli wa miaka mingi kuwa kupika au kutumia moto katika kuandaa vyakula kunaharibu virutubisho vya asili vinavyopatikana katika mbogamboga.

Mbogamboga zinaondoa tindikali inayozalishwa wakati vyakula vingine vikisagwa tumboni kama vile nyama na jibini. Mboga za majani za kijani ni chanzo kikubwa cha carotene ambayo inabadilishwa mwilini na kuwa vitamini A. pia, ni chanzo kizuri cha vitamini C.

 

Vitamini A ina kazi kubwa ya kuimarisha macho ili yaone vizuri hasa wakati wa giza na ndiyo maana wapo wanaoshauri kula mchicha kwa wingi kama hawaoni vizuri hasa kama giza limeingia. Vitamini A. Mbogamboga pia, inasaidia pia ukuaji na ufanyaji kazi wa chembehai na kuimarisha kinga ya mwili.

Vitamini C ina kazi nyingi ikiwemo kuimarisha ufanyaji kazi wa chembehai, inaimarisha kinga, kuponya mafua na vidonda. Baadhi ya mbogamboga zina protini na wanga. Kwa mfano, maharage na kunde ni chanzo kikubwa cha madini ya chuma na protini.

Makala haya imeandikwa na mtaalam wa Lishe, Abdallah Mandai. Kwa ushauri unaweza kuwasiliana nae kwa namba hizo hapo juu.

Mawasiliano Simu namba 0716 300 200, 0754 391 743.

Comments are closed.