Kartra

Ulinzi Waimarishwa Simba Vs Yanga

UONGOZI wa Uwanja wa Benjamin Mkapa umefunguka kuwa maandalizi yote kuelekea mchezo wa Dabi ya Kariakoo utakaozikutanisha Simba na Yanga Jumamosi hii yamekamilika na kujinasibu kuwa kuelekea mchezo huo ulinzi utaimarishwa.

 

Simba na Yanga Jumamosi hii zitakutana katika mchezo wa Dabi ya Kariakoo, kwenye mzunguko wa pili wa ligi ambao unatarajiwa kuanza majira ya saa 11:00 jioni.

 

Wababe hao kutokea viunga vya Kariakoo wataingia katika mchezo huo wakiwa na kumbukumbu nzuri ya sare, katika mchezo wa mzunguko wa kwanza uliochezwa Novemba 7, mwaka jana.

 

Akizungumza na Championi Jumatano,Godwin Nsajigwa ambaye ni meneja wa uwanja huo, alisema: “Kwa ujumla uwanja wetu wa Mkapa utakaotumika katika mchezo wa Jumamosi kati ya Simba dhidi ya Yanga uko vizuri, tunaendelea na marekebisho madogomadogo ambao ni utaratibu wa kila siku wa kiutunzaji.

 

“Ndani ya siku tatu zilizosalia tunatarajia kuwa na vikao vitatu vya kamati ya ulinzi na usalama ambavyo lengo lake ni kuhakikisha miundombinu ya uwanja na mashabiki wote wanaokuja kutazama mchezo huo, wanakuwa salama ndani na nje ya uwanja na mchezo unaisha bila matatizo yoyote.”

Stori: JoeL Thomas, Dar es SalaamToa comment