Umri Wamtesa Samatta Genk

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta ameonyesha kujuta kwake kuchelewa kuingia Ulaya kucheza soka la kulipwa baada ya kusema alitamani kuona anacheza soka majuu mapema kabla ya kufikisha umri wa miaka 18.

 

Samatta ambaye anacheza soka la kulipwa kwenye Klabu ya KRC Genk ya nchini Ubelgiji, ametoa kauli hiyo ikiwa ni muda mchache baada ya kuisha mchezo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Ulaya kati Genk na Red Bull Salzburg ya Austria huku Genk ikichezea kichapo cha mabao 6-2, Samatta akifunga bao la pili kwa Genk.

TA

Samatta ambaye pia ni nahodha wa Taifa Stars ameingia Ulaya akiwa na miaka 24 baada ya kujiunga na KCR Genk mwaka 2016 akitokea TP Mazembe ya DR Congo kitu ambacho anaamini kimemchelewesha kutokana na rekodi anazoendelea kuweka. Kupitia akaunti yake ya mtandao wa kijamii wa Instagram, Samatta aliandika kuwa: “Tujadili kidogo.

 

Ni jambo gani unatamani lingetokea katika maisha yako mapema? “Mimi natamani ningekuwa katika soka la Ulaya kabla hata sijafika 18,” huku akitoa msisitizo kuwa hakosoi mipango ya Mungu. Ikumbukwe mshambualiaji huyo ameweka rekodi nyingi ikiwemo ya kuwa Mtanzania wa kwanza kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya na kufunga bao katika mchezo wake wa kwanza kucheza


Loading...

Toa comment