The House of Favourite Newspapers

Unajua athari za kuitana sweet na dear wakati siyo wachumba?

0

healthycouple-lifemagASALAM alaikum wapenzi wasomaji wangu, kwa waliobomolewa nyumba poleni sana msife moyo wa kutafuta zaidi bila shaka Mungu ana kubwa la kuwapa.

Baada ya kuwapa pole sasa niingie kwenye mada yetu moja kwa moja kwani limekuwa ni tatizo kubwa hasa kwa wanawake kumuita kila mtu jina la mpenzi mara dear, sweetheart na mengine kibao mtu ambaye hana uhusiano naye wa kimapenzi.

Majina haya yana sehemu maalum ya kutumika, hata kwa wenye wapenzi wao wanaowaita majina haya huwa yana sehemu maalum ya kutumika si kila sehemu.
Mfano mkiwa ofisini, huwezi kumuita mke au mpenzi wako majina haya, hapo ni sehemu ya kazi mnaitana majina yenu kama kawaida.

Majina haya mara nyingi hutumika nyumbani, mkiwa kwenye gari au hata sehemu ya shughuli mbalimbali, mkiwa na watu ambao hawahusiani na kazi.

Mfano: Dear, naomba uniamshe saa 12:00 asubuhi, kesho nina vikao vingi sana asubuhi, inaweza kuwa kauli ya mume akimwambia mkewe, ambaye naye anamjibu: Sawa sweet, usijali.

700-love-couple-relationship-kiss-passion-sex-marriage-dateAu: Mpenzi nimechoka naomba uninyooshee nguo zangu kesho nahitaji kuwahi mapema, au love nimekupangia chakula karibu mezani.

Nadhani mnaona jinsi majina hayo yanavyopendeza hapo, au ni rahisi sana kulitumia kwenye ujumbe wa meseji (SMS) lakini kwa mumeo au mpenzi wako tu.

Mada hii nimeamua kuiandika kwenu kwa sababu naona siku hizi hata majirani mnaamua kuwaita wapenzi, utasikia mama f’lani kaamka asubuhi anakwambia mpenzi umeamkaje, au kwenye simu anaongea na shosti wake anamuita mpenzi.

Sasa unawezaje kutofautisha mpenzi mume na mpenzi jirani au rafiki, huoni kama unampunguzia mumeo mahaba? Hii ni mbaya sana, wanawake siku hizi mmejisahau sana katika hili.

Athari zake
Kubwa zaidi hupunguza mahaba kwani jina mojawapo katika hilo unapokuwa unamuita mume au mpenzi wako linabeba ujumbe f’lani na hasa mwanamke unapomuita mpenzi wako jina hilo hujikuta ukideka kidogo, kudeka kule ndiyo hasa humvuta mume.

Nyingine siku hizi ukimuita mpenzi wako baby au sweet anaona kuwa unamuibia kwani amezoea kuitwa majina hayo na watu wasiokuwa wapenzi wake, hivyo majina haya yamepoteza thamani kwa ujumla.

Ni rahisi mpenzi
wako kukusaliti
Kutokana na majina haya ni rahisi mpenzi wako kukusaliti kwani ukiwakuta wote wanaitana mpenzi utajua ni jina tu kama ulivyozoea lakini wapo wanaoitana hivyo na kumbe wameshaanzisha uhusiano wa kimapenzi hivyo wakati mwingine unahitaji kuwa makini na umpendaye.

Wengine huwaita hata wanawake wenzao hivyo wewe unaweza kuona kuwa anayeitwa hivyo ni mwanamke na kumchukulia poa lakini kumbe wameshakuwa na uhusiano usiofaa.

Leo nimekuwa mpole sana katika mada hii ili muelewe wasomaji wangu, mnayajua vizuri makali yangu hasa ninapowapa somo. Kwa leo naishia hapa, tuonane wiki ijayo.

Leave A Reply