The House of Favourite Newspapers

unamnyima unyumba mumeo wivi wa nini?

0
Portrait of unhappy woman arguing with man in bedroom

Asalam Alaikum mpenzi msomaji wangu, bila shaka unaendelea vema kwa upande wangu namshukuru Mungu naendelea vema na ndoa yangu inasonga.

Leo nimekuja kuongea na wanawake wenzangu mnaowanyima unyumba waume zenu lakini cha kushangaza mnawaonea wivu hamtaki hata wawasalimiane na majirani wa kike, je huko ni kuwapenda au roho mbaya?
Kwa muda mrefu nimekuwa nikishea na nyinyi wasomaji wangu mawazo yenu na matatizo yenu ya kiuhusiano ambayo huwa nayajadili kwa faida ya wote.

Mada yetu hii ya leo imekuja baada ya kutumiwa ujumbe na msomaji wangu mmoja ambaye aliandika;
“Mambo dada Chau, mimi ni kijana niliyebahatika kuoa lakini cha kushangaza mke wangu kwa sasa amebadilika, kila nikihitaji unyumba mpaka nimlazimishe, kibaya zaidi ana wivu balaa hata nikisalimiana na mwanamke mwingine kwake ni shida anasema ni mwanamke wangu. Nisaidie nifanyeje kwa mtu huyu?”

Hivi wanawake mnaofanya kama huyu shoga yetu mnakuwa na tatizo gani? Kwa nini umtese mumeo na kama humtaki kwa nini usimuache akaenda kwa mwingine.

Swali la kujiuliza wewe unapewa na nani unyumba mpaka unashindwa kushiriki na mwenzako? Au ndiyo unamfanya mtumwa wako halafu wewe unapata faraja kwa mtu ambaye bado hujamuweka wazi hivyo unatafuta visa ili upate sababu ya kuachana na mumeo?

Wanawake wenzangu ndoa ni jambo la kuheshimika kwa sababu wapo wanaoililia na hawaipati,  ili ndoa iitwe ndoa unyumba ndiyo kiungo kikubwa sasa wewe unayemnyima mwenza wako unyumba utasema uko kwenye ndoa kweli au upo kwenye urafiki?

Mwanamke anapofikia hatua ya kulalamika mpaka kwa watu ujue kuwa hana muda mrefu atakubwaga tu je, mwanamke kuachwa kwa sababu ya kitu hicho huoni kuwa ni kashfa, je, ukienda kwa mwingine utampa unyumba kama kawaida au ndiyo utamaliza majumba?

Wanawake wengi mkishaingia kwenye ndoa kiukweli mnajisahau sana na kuona kuwa ndiyo mmefika kisa tu ndoa, sasa kitendo cha ndoa kisikufanye wewe ukamfanyia chochote mumeo, dunia ya sasa imebadilika sana unaweza kuachwa kwa sababu ndogo tu ndoa isiwe kigezo kabisa.

KUNUNUA NA KUSOMA MAGAZETI YA GLOBAL PUBLISHERS ONLINE, INGIA HAPA==>VODACOM M-PAPER APP

*********

JIUNGE NA SOCIAL MEDIA ZETU

KWA HABARI ZA KITAIFA, KIMATAIFA, MASTAA NA MIKASA YA KUSISIMUA

INSTAGRAM: @Globalpublishers

ERIC SHIGONGO INSTAGRAM: @ericshigongo

TWITTER: @GlobalHabari

FACEBOOK: @GlobalPublishers

SUBSCRIBE YOU TUBE: Global TV Online

GLOBAL TV ONLINE: www.globaltvtz.com

HADITHI ZA KUSISIMUA NA MBINU ZA UJASIRIAMALI, ERIC SHIGONGO FACEBOOK PAGE:@shigongotz

Leave A Reply