The House of Favourite Newspapers

Uncle Shamte: Natamani Nishuhudie Diamond Akioa

0

MUME wa mama mzazi wa Diamond Platnumz, Mama Dangote ambaye anajulikana zaidi kwa jina la Uncle Shamte anasema amekuwa akiulizwa maswali wengi kuhusu uhusiano wa mwanawe huyo wa kambo malkia mpya wa Bongo Fleva, Zuchu.

 

Hata hivyo, amekuwa akijibu kwa kifupi kwamba itajuliakana Februari 14 (leo) akisema itakuwa siyo siku ya kawaida hata kidogo.

Uncle Shamte anasema kuna jambo kubwa litakalotendekea Valentine hii na itafahamika kama ni kweli Diamond anakusudia kufungua ndoa na Zuchu.

“Swali kama tulipeleka barua ya uchumba litajibiwa tarehe 14 (leo). Mimi siyo muongo, kuna tukio kubwa linakwenda kutokea tarehe 14 ambalo linamhusu Zuchu,” anasema Uncle Shamte.

 

Hivi majuzi uvumi uliibuka kuwa baba huyo wa kambo wa Diamond aliandamana na kaka wa jamaa huyo, Ricardo Momo pamoja na wazee kadhaa kutoka upande wa Diamond kupeleka barua ya uchumba nyumbani kwa kina Zuchu kama mojawapo ya maandalizi ya harusi kati ya wasanii hao wawili.

 

Uncle Shamte anasema kuwa anatamani sana kumwona Diamond akifunga pingu za maisha huku akieleza kuwa atakuwa na furaha kubwa siku ambayo atapiga hatua hiyo.

 

“Furaha itapitiliza. Furaha huwa haijifichi, mtaiona. Mimi binafsi natamani nishuhudie Diamond akioa kwa sababu namjua mwanangu. Napenda nimuone akifanya jambo hilo,” anasema Uncle Shamte.

STORI; SIFAEL PAUL, DAR

Leave A Reply