The House of Favourite Newspapers

UNI-INDUSTRIES KUMWAGA OFA ZA NGUVU KWENYE MAONESHO YA BIASHARA

 

Kampuni inayoongoza kwa uuzaji wa bidhaa bora za uokaji mikate na keki, mashine za kufulia nguo, majokofu na vifaa mbalimbali vya jikoni pamoja na huduma za catering, wanatarajiwa kuwa kivutio kikubwa kwenye maonesho ya vifaa vya huduma mbalimbali ya Africa Premier Food Service and Equipment Pro, yanayotarajiwa kufanyika kwa siku mbili kuanzia Agosti 6 hadi Agosti 7 mwaka huu.

 

Maonesho hayo maalum, yatafanyika kuanzia saa tatu asubuhi hadi saa kumi na moja jioni, kwenye ofisi za kampuni hiyo zilizopo Barabara ya Haile Selasie, Mkabala na Marrybrown, Masaki jijini Dar es Salaam ambapo vifaa vyenye ubora wa kimataifa katika uokaji wa mikate, keki na vyakula mbalimbali, vinavyozalishwa na kampuni kubwa ya Mac Adams vitaoneshwa.

 

Bidhaa nyingine ni pamoja na vifaa vyote vya kisasa kwenye majiko ya kibiashara, kuanzia mahotelini na kwenye migahawa mikubwa, vifaa maalum vya kutolea huduma za catering na majokofu ya kisasa yanayotumia umeme kidogo.

 

Pia wateja watapata punguzo la bidhaa mbalimbali, litakaloendana na huduma za kudizainiwa mpangilio wa vifaa hivyo kwa wateja, usafiri wa kuvipeleka mpaka nyumbani kwa mteja na kufungiwa bure.

Kwa maelezo zaidi, unaweza kuwapigia simu kwa namba 0766 075 031 au tembelea mtandao wao kwa kubofya www.uni-eastafrica.com au www.uni-onlineshop.com .

Comments are closed.