The House of Favourite Newspapers

Upanuzi Anglo Gold Ashanti Kuimarisha Mahusiano Uchimbaji Nchini

0

Kwa kuzingatia mpango wa kuongeza mchango endelevu katika uchumi wa jamii inayozunguka mgodi, Kampuni ya Anglogold Ashanti imeingia ubia na kampuni ya BG Umoja ya nchini Tanzania na kuipatia mkataba wenye thamani ya dola za Marekani milioni 186 kwa ajili ya miradi ya uchimbaji ya Nyankanga na Geita Hill katika kipindi cha miaka miwili.

 

 

Ubia huo wa asilimia 80/20 ni ushirikiano baina ya kampuni ya Africa Underground Mining Services (AUMS) ya Tanzania, kampuni tanzu ya kundi la Perenti Australia na kampuni ya huduma za uchorongaji wa ndani na usambazaji madini ya Geofields Tanzania Limited.

 

 

Ushirikiano huo utafanyika sawa na muundo wa ushirikiano uliotekelezwa katika uchimbaji wa chini kwa chini katika Mgodi wa Obuasi nchini Ghana kati ya AUMS Ghana na Kampuni iliyopo Accra – inayomilikiwa na Waghana ya Rocksure, ushirikiano utakaojenga uwezo wa uchimbaji maalumu ndani ya nchi.

 

 

Akizungumzia ubia huo Afisa Uendeshaji Mkuu wa AngloGold Ashanti –Afrika, Sicelo Ntuli alisem; “Tunafanya kazi na wakandarasi wa uchimbaji wenye uzoefu watakaotusaidia kuwezesha uhamisho wa muda mrefu wa ujuzi endelevu, na kuendelea kujenga mipango endelevu ya manunuzi ya ndani.

 

“AngloGold Ashanti inajenga mipango endelevu ya manunuzi ya ndani itakayochochea maendeleo ya uchumi na jamii katika miradi, inayoshuhudiwa na mchango mkubwa kutoka Geita Gold Mining Limited ambao umechangia mapato makubwa ya watu wa Tanzania.”

 

 

Alisema matumizi ya mwaka ya AngloGold Ashanti kwa watoa huduma Watanzania wazawa yameongezeka hadi dola milioni 162 kuanzia mwaka 2016.

 

 

”Timu ya kusimamia manunuzi ya ndani imejiwekea malengo makubwa ya asilimia 60 hadi 70 ya matumizi yote kufanywa na kampuni za Kitanzania nchi ifikapo 2025.

 

 

” Kampuni ya AngloGold Ashanti – Geita Gold Mining Limited imetoa pia mkataba wa miaka miwili wa usafirishaji mafuta wenye thamani ya dola milioni 10.8 kwa mwaka kwa kampuni mbili za Kitanzania. Mojawapo ya kampuni kati ya mbili zitakazonufaika katika mkataba huo ina asili ya Geita na inathibitisha ahadi ya GGML kuwezesha uchumi wa jamii wenyeji,” alisema.

 

 

Alisema kampuni ya Geita itakayonufaika katika mpango huo imepatikana baada ya jitihada za GGML kushirikiana na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) kutoa mafunzo wezeshi kwa watoa huduma wa Geita ili kuongeza wigo wa kushindana katika manunuzi na utoaji huduma unaofanywa na Mgodi.

 

”Katika kufikia viwango vya kimataifa, malori ya kubeba mafuta hayo yamepewa mwongozo wa kuzingatia utoaji moshi kwa mujibu wa viwango vya EURO IV, matangi yanapaswa kutengenezwa kwa kutumia aluminium ili kupunguza uzito na kila gari litapaswa kutumika katika kipindi kisichozidi miaka sita.

 

 

” Wakandarasi katika mpango huo wamekwishaajiri madereva wa malori wanawake ili kukidhi mahitaji ya mgodi kwenye masuala ya utofauti na ujumuishaji. Wakandarasi wote wanaendelea na jitihada mbalimbali za kunufaisha jamii inayozunguka mgodi”.

NA MWANDISHI WETU

Leave A Reply