The House of Favourite Newspapers

Updates: Waliofariki MV Nyerere Wafikia 126 – Video

16:00 – Idadi ya miili iliyoopolewa yafika 126
Idadi ya miili iliyoopolewa kwenye kivuko cha Mv Nyerere imefikia 125 mpaka sasa

 

12:49 – IGP SIRRO: UTAMBUZI WA MAREHEMU UNAENDELEA
Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Simoni Sirro amesema utambuzi wa marehemu katika ajali ya MV Nyerere mkoani Mwanza unaendelea kwa miili iliyoopolewa.
Litafunguliwa Jalada maalum la kuchunguza tukio la kuzama kwa kivuko cha MV. Nyerere

 

12:40 – MIILI ILIYOOPOLEWA YAFIKA 100
Miili ya waliokufa na kuopolewa mpaka sasa yafika 100.

 

11:41 – IDADI YA WALIOOPOLEWA YAFIKA 94
Idadi ya vifo katika ajali ya kivuko cha MV Nyerere, Mwanza imefika watu 94 huku uokoaji ukiendelea, RC John Mongella amethibitisha

 

10:40 – MIILI 86 IMESHAOPOLEWA MPAKA SASA
Idadi ya vifo katika ajali ya kivuko cha MV Nyerere, Mwanza imefika watu 86 huku uokoaji ukiendelea, RC John Mongella amethibitisha

ZOEZI la uokoaji wa miili ya watu waliozama katika ajali ya Kivuko cha MV Nyerere linaendelea muda huu ambapo vikosi maalum vya uokoaji vya Jeshi la Polisi, JWTZ , Jeshi la zimamoto na uokoaji na wazamiaji kutoka kampuni ya huduma za ndege Mwanza kusitisha zoezi jana usiku kutokana na ukosefu wa vifaa vyenye uwezo wa kufanyakazi kwenye giza.

 

KWA mujibu wa HABARI ZA MIKOANI kutoa TBC 1, imeelezwa kuwa mpaka leo asubuhi, waliookolewa wakiwa wamepoteza maisha idadi yao imeongezeka na kufikia 79.

 

Mpaka jana usiku, watu 44 walikuwa wameokolewa wakiwa wamepoteza maisha huku 37 wakiwa majeruhi lakini hali zo zilikuwa mbaya.

Updates:

RC wa Mwanza, John Mongela amesema idadi ya watu waliofariki kwa ajli ya kuzama Ziwa Victoria imeongezeka na kufikia 94 leo asubuhi. DC Ukerewe amesema Kivuko kilikuwa na uwezo wa kubeba abiria 100 na tani 25 za mizigo, lakini kibeba abiria zaidi ya 400.

 

Vikosi vya uokoaji mkoa wa Mwanza vimeongezewa nguvu na vikosi vya mkoa wa Mara katika eneo la tukio kuongeza kasi ya kuokoa na kuopoa watu waliopinduka na kivuko hicho. Mkuu wa Jeshi la polisi IGP Simon Sirro na Waziri wa Uchukuzi Isaac Kamwelwe wamefika eneo la tukio kushiriki uokoaji.

 

Wakati uokoaji na uopoaji ukiendele mamia ya wakazi wa visiwa hivyo wamefurika kituo cha afya cha Bwisya kutambua jamaa zao walioopolewa. Tayari uongozi wa wakala wa meli mkoa wa Mwanza umetambua wafanyakazi wa kivuko watano ambao wamepoteza maisha akiwemo   nahodha, fundi, Karani, mlinzi na mkuu wa kivuko, Kivuko hicho kilikuwa na wafanyakazi wanane.

 

TAZAMA VIDEO MIILI IKIOKOLEWA

Comments are closed.