The House of Favourite Newspapers

Upelelezi wa Kesi ya Scorpion Wakamilika, Kuanza Kusikilizwa Novemba 30

DAR ES SALAAM: Upelelezi wa kesi ya kudaiwa kumtoboa macho, kumjeruhi tumboni na kumpora fedha na mkufu Said Mrisho inayomkabili mkazi wa Machimbo Yombo jijini Dar es Salaam, Salum Njwele (34) maarufu kama Scorpion umekamilika na kesi inatarajiwa kuanza kusikilizwa Novemba 30, mwaka huu.

mahakamaniScorpion (aliyefungwa pingu) akielekea kwenye chumba cha mahakama.  

Hayo yamesemwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala leo  na Hakimu Flora Lymo anayesikiliza kesi hiyo.

Wakati wa kesi hiyo, mtuhumiwa Scorpion aliomba asomewe maelezo ya awali lakini hakimu Lymo alikataa.

scopioni-1-2

Gari la polisi likimsubiri nje kwa ajili ya kumrudisha lupango.

Scorpion anadaiwa kutenda makosa hayo Septemba 6, mwaka huu eneo la Buguruni Sheli wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam ambapo anatuhumiwa kuiba mkufu rangi ya fedha wenye uzito wa gramu 34 ukiwa na thamani ya Sh 60,000, bangili na fedha taslimu Sh 331,000 vyote kwa pamoja vikiwa na thamani ya Sh 476,000 mali ya Mrisho.

scopioni-1-3

Scorpion akiwa ndani ya gari la polisi.

Wakati wa kusikilizwa kesi hiyo iliyovuta hisia nyingi za watu hususani wakazi wa jijini Dar ulinzi ulikuwa mkali muda wote.

Global Halotel

Comments are closed.