The House of Favourite Newspapers

Urusi Yasaini Mkataba na Kampuni ya Dubai DP World Bahari ya Arctic

0

Serikali ya Urusi imesaini Mkataba na Kampuni ya Dubai DP World ili kushirikiana na Kampuni iliyo chini ya Serikali ya Urusi katika shughuli za usafirishaji katika Bahari ya Arctic.
Urusi ambayo inataka kunufaika na fursa ya mabadiliko ya hali ya hewa huko Kaskazini ya Mbali imeingia dili na kampuni hiyo kubwa ya usafirishaji na bandari yenye makao yake makuu Dubai unaolenga kusaidia kudhibiti shughuli kwenye njia za Bahari ya Arctic.
Wakati mabadiliko ya hali ya hewa yakileta maafa kwa sehemu kubwa ulimwenguni msimu huu wa joto ikiwa ni pamoja na mafuriko, moto na mawimbi ya joto, mradi huu wa Urusi unafikiria kutumia kuyeyuka kwa barafu ya Arctic kama ‘kuua ndege wawili kwa jiwe moja’.
Kwanza kutapunguza uchafuzi wa hali ya hewa kwa kuwa matumizi ya viyeyusha barafu (icebreaker) yatapungua na kurahisisha safari kati ya Asia na Ulaya jambo ambalo DP World imehimiza kushirikiana katika kukiendeleza.
Akizungumzia uamuzi wake wa kuwekeza katika njia ya bahari ya Urusi, mwenyekiti na mtendaji mkuu wa DP World, Sultan Ahmed Bin Sulayem, amesema “kilichotusukuma ni kuyeyuka kwa barafu”
Ingawa barafu bado inaziba Njia ya Bahari ya Kaskazini muda mwingi wa mwaka, sasa vyombo vilivyoundwa kwa kiwango cha kukabiliana na barafu vitafanya shughuli zao mara kwa mara na vitasafiri umbali mrefu bila kutegemea usaidizi wa ice-breaker wakati wa kiangazi.
Chini ya mpango huo, DP World na kampuni ya Urusi ya Rosatom inayosimamia Njia ya Bahari ya Kaskazini, wataunda kundi la meli za kontena za kiwango cha barafu.

#EXCLUSIVE: DINAMITE BINTI (12) ANAYEISHI ITALI – ”DIAMOND NAMPENDA, KUPIKA SIJUI ILA KULA NAJUA”


 

Leave A Reply