The House of Favourite Newspapers

Kocha Mkuu wa Simba Ashtukia Jambo Ligi ya Mabingwa Afrika

0
Kocha wa Kikosi cha Simba.

MARA baada ya kuwa na uhakika wa kuvaana na kikosi cha Power Dynamos katika mchezo wa hatua ya pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Kocha Mkuu wa Simba Mbrazili, Roberto Oliviera ‘Robertinho’ ameshtukia jambo na kuweka wazi kuwa utakuwa mchezo mgumu kwani timu zote mbili zilisomana kupitia mchezo wa kirafiki wa Simba Day.

Simba na Power Dynamos walikutana kwenye mchezo wa kimataifa wa kirafiki wa kilele cha Simba Day, Agosti 6 mwaka huu ambapo Simba walifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 yaliyofungwa na mastaa wao wapya Fabrice Ngoma na Willy Onana.
Power Dynamos ambao ni mabingwa watetezi wa Zambia wanatarajiwa kuvaana na Simba katika hatua ya pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika, baada ya kufanikiwa kusonga mbele kwa kuitoa African Stars ya Namibia.
Power Dynamos imevuka hatua hiyo baada ya matokeo ya jumla ya sare ya mabao 2-2 dhidi ya African Stars, huku faida ya bao la ugenini ikiwabeba.
Simba ni miongoni mwa timu nane ambazo zilipata faida ya kuanzia hatua ya pili kutokana na idadi ya pointi nyingi walizokusanya kwenye viwango vya Shirikisho la soka Afrika (CAF), na sasa wanatarajia kuvaana na Dynamos kwa kuanzia ugenini kati ya Septemba 15 hadi 17, mwaka huu.
Akizungumza na Championi Jumatatu, Robertinho alisema: “Tunatarajia mchezo mgumu kwa kuwa tulikutana nao Simba Day, lakini tupo tayari kama kikosi kuona tunafuzu hatua ya mtoano.”

Stori na Joel Thomas

KUMBE MZEE WA KULA CHUMA HICHO NI MCHAMBUZI BORA WA BOLI, TAZAMA ALIVYOICHAMBUA YANGA YA PACOME…

Leave A Reply