The House of Favourite Newspapers

Urusi Yawaachilia Wageni 10 Waliotekwa Ukraine Baada ya Upatanishi wa Saudia

0
Mwanamfalme wa Saudia Mohammed bin Salman

URUSI siku ya Jumatano iliwaachilia huru wafungwa 10 wa kigeni wa vita waliokamatwa nchini Ukraine kufuatia upatanishi wa Mwanamfalme wa Saudia Mohammed bin Salman, wizara ya mambo ya nje ya Saudia ilisema.

 

Wafungwa walioachiliwa ni raia wa Marekani, Uingereza, Croatia, Morocco na Sweden, wizara hiyo ilisema katika taarifa yake na kuongeza kuwa ndege iliyowabeba wafungwa hao ilitua katika ufalme huo.

 

“Mamlaka husika ya Saudi ilipokea na kuwahamisha kutoka Urusi hadi kwa ufalme na inawezesha taratibu za nchi zao,” ilisema taarifa hiyo.

Mbunge wa Uingereza Robert Jenrick

Wizara haikutambua wafungwa hao Afisa mmoja wa Saudia alisema walikuwa Waingereza watano, Wamarekani wawili, Mkroatia, Mmorocco na raia wa Uswidi.

 

Mbunge wa Uingereza Robert Jenrick alisema Aiden Aslin ni miongoni mwa walioachiliwa, alikamatwa mapema mwaka huu kisha akahukumiwa kifo na mahakama katika jimbo linalojiita Donetsk People’s Republic (DPR), moja ya washirika wa Urusi mashariki mwa Ukraine.

 

Imeandikwa: leocardia Charles kwa msaada wa mitandao.

Leave A Reply