Ushirikiano Wa Kimkakati Kati Ya Benki Ya Stanbic Na Ramani.io Kuboresha Sekta Ya Biashara Nchini
Dar es Salaam, Tanzania, 22/04/2024. Benki ya Stanbic Tanzania ambayo ni kiungo muhimu katika sekta ya huduma za kibenki nchini Tanzania, na Ramani, kampuni namba moja kwenye teknolojia ya kifedha wanafurahi kutangaza ushirikiano katika mkakati uliolenga kuleta mabadiliko kwenye sekta ya biashara na kuendeleza upatikanaji wa huduma za kifedha nchini Tanzania kwa ufanisi zaidi. Ushirikiano huu wakipekee unalenga kutumia teknolojia na msaada mkubwa wa kifedha, kuimarisha uwezo wa biashara za wasambazaji wa ndani na wajasiriamali.
Muunganiko huu unalenga kutumia miundombinu ya kifedha ya kisasa ya Ramani, pamoja na rasilimali imara za kifedha za Benki ya Stanbic. Pia, utasaidia zaidi ya wasambazaji 100 katika mwaka wake wa kwanza, ukiangazia mnyororo muhimu wa thamani katika sekta ya Bidhaa za Watumiaji (FMCG).
Pamoja na majukwaa ya teknolojia ya hali ya juu na mikakati ya kifedha, ushirikiano huu utakabiliana na vipengele muhimu vya usimamizi wa biashara, ufuatiliaji wa mauzo na miamala ya kidijitali ili kuongeza ufanisi wa uendeshaji kwa wasambazaji.
Fredrick Max, mkuu wa kitengo cha biashara wa Benkiya Stanbic Tanzania, alisema, “Ushirikiano wetu na Ramani ni zaidi ya biashara; ni ushirikiano wa kimkakati ambao unaahidi kubadilisha jinsi biashara inavyofanywa nchini Tanzania. Kwa kuunganisha nguvu zetu na maono yetu, tunapanga kusaidia mahitaji ya kifedha ya wasambazaji wa ndani na pia kuchangia kwa kiasi kikubwa katika ukuaji wa uchumi wa taifa letu.”
Lengo kuu ni kutoa fedha kwa wasambazaji na wauzaji ili kuboresha usimamizi wa ugavi kwa wasambazaji na wafanyabiashara wa bidhaa kubwa kama Coca-Cola. Hii itawezesha usimamizi bora wa manunuzi, udhibiti wa hisa, na ufuatiliaji wa mauzo ya kidijitali, katika kuimarisha michakato ya biashara na miamala ya kifedha.
Iain Usiri, Mkurugenzi Mtendaji wa Ramani, alisema; “Tunafurahi kushirikiana na Benki ya Stanbic Tanzania. Ushirikiano huu utarahisisha na kuimarisha usimamizi wa wasifu wa mikopo, na kukuza huduma za kifedha. Tunaleta mabadiliko chanya katika kuendesha biashara, na kuboresha upatikanaji wa huduma za kifedha.”
Uzinduzi rasmi wa ushirika huu ulifanyika katika hoteli ya Hyatt Regency mnamo Aprili 22, 2024. Tukio hilo lilijumuisha hotuba kuu kutoka kwa watendaji wa mashirika yote mawili, mijadala mbalimbali na kipindi cha maswali na majibu kilicholenga kushirikisha wadau waliohudhuria na vyombo vya habari. Uzinduzi huu haukulenga kuzindua mkakati huu mpya wa biashara, bali pia ilikuwa fursa ya kushirikiana moja kwa moja na wadau wote waliohudhuria.
Mafanikio ya ushirikiano huu yatapimwa na uandikishwaji wa wafanyabiashara 100 katika mwaka wa kwanza na mipango ya kukuza ufikiaji kwa kiasi kikubwa ili kufikia biashara zaidi nchini Tanzania.
Takwimu za mitandao ya kijamii, ukuajiwakifedha, na viwango vya kuandikisha wateja, zitatumika kama viashiria muhimu vya mafanikio na ufanisi wa muunganiko huu.
Ushirikiano kati ya Benki ya Stanbic Tanzania na Ramani, unatengeneza kiwango kipya cha ushirikiano katika sekta ya kifedha na teknolojia, huku ukionyesha matumaini makubwa katika kuboresha jinsi biashara inavyofanywa na kusaidiwa kifedha nchini Tanzania.
Kupitia hatua hii, mashirika yote mawili yanathibitisha tena azma yao ya kuchochea ukuaji wa kiuchumi na kuboresha upatikanaji wa huduma za kifedha kwa Watanzania wote.
KuhusuBenkiya Stanbic Tanzania
Benki ya Stanbic Tanzania ni sehemu ya Benki ya Standard, muunganiko mkubwa zaidi wa benki barani Afrika kwa mali na mapato. Ina azimio kuu la kukuza suluhisho za kifedha ambazo zitaendeleza ukuaji wa kiuchumi nchini Tanzania.
Kuhusu Ramani.io
Ramani.io ni kampuni ya teknolojia ya kifedha inayoongoza nchini Tanzania, iliyoanzishwa ili kutoa miundombinu imara ya kifedha inayosaidia mnyororo wa thamani na kuimarisha shughuli za kiuchumi nchini kote.