The House of Favourite Newspapers

Usidanganyike, ni Kweli Inatolewa

0

10.Mdau wa Gazeti la Championi,Neema Steven akijaza kuponi yake ili kushiriki Bahati nasibu ya Shinda Nyumba. ASUBUHI ya Julai 9, 2003 kijana mwenye umri wa miaka 36, Teddy LeBarge kutoka Snellville, nchini Marekani, hakuamini masikio na macho yake, alipoambiwa kuwa alikuwa ni mshindi wa dola milioni 193 (bilioni 386) katika Bahati Nasibu kubwa iliyofanyika nchini humo.

Na hii haikumtokea kwa bahati mbaya Teddy, kwani kwa mujibu wa ushuhuda wake baadaye, alikuwa ni mwenye tabia ya kucheza kila bahati nasibu iliyotokeza mbele yake, kwa kuwa aliamini kama kuna mtu anashinda kweli, basi ipo siku mshindi huyo anaweza kuwa yeye.

Teddy ambaye hakupata elimu ya kutosha kama Wamarekani wengi walivyo, anasimulia kisa cha kusisimua.

3.Rehema Said (kulia) mkazi wa maeneo ya Mbande akishiriki kujaza kuponi ili kuingia katika droo ya Shinda Nyumba.“Yeah, ilikuwa ni kawaida yangu kila Ijumaa lazima niende kwenye kituo cha mafuta cha Amoco ambako kuna michezo mingi ya kubahatisha inayochezwa. Nilinunua tiketi za michezo ile midogomidogo, lakini sikusahau kununua ile ya droo kubwa iliyokuwa ikichezwa, kwa sababu nilijua huko ndiko ninakoweza kupata hela kubwa. Kuna wakati niliona ni kupoteza muda na huenda sitashinda, lakini sikukata tamaa, niliendelea kununua tiketi kila siku.”

Hii siyo hadithi, bali ni simulizi ya kweli iliyotokea kule Marekani, miaka 13 iliyopita na sasa jambo kama hili linatokea Tanzania, ambapo Kampuni ya Global Publishers & Enterprises Ltd, inamtafuta mtu ambaye Juni 30, mwaka huu atakuwa ni mshindi wa droo kubwa kabisa kuwahi kutokea ya Shinda Nyumba, ambaye atapewa mjengo wenye thamani ya shilingi milioni 60, ukiwa na kila kitu ndani yake.

Huwezi kujua, mtu huyo anaweza kuwa wewe unayesoma makala haya hivi sasa, kwani kama umekuwa ukinunua tiketi yako kila mara, endelea kwa sababu atakayeshinda anaweza kuwa ni atakayenunua tiketi yake leo. Na kama hujawahi kununua kuponi, hujachelewa, huenda wewe ndiye unasubiriwa.

Ni kama simulizi, maana haijawahi kutokea kwa kampuni ya magazeti nchini kutoa zawadi kubwa kama hiyo. Huna sababu za kutoamini kwa sababu kabla ya hapo, Global Publishers imeshafanya mengi yanayofanana na hayo.

Imewahi kutoa zawadi kubwa za magari kama Mercedes Benz, Toyota Prado, Toyota Noah, Toyota Vitz na Fun Cargo, achilia mbali zawadi kama pikipiki za kila aina, vyombo vya nyumbani, seti za televisheni za kisasa na vitu vingine kedekede.

Magazeti ya Global Publishers ambayo yana kuponi za kuweza kukufanya kuwa mmoja kati ya wamiliki wa nyumba ya thamani kubwa katika Jiji la Dar es Salaam ni Uwazi, Championi, Ijumaa, Ijumaa Wikienda, Risasi Mchanganyiko, Risasi Jumamosi na Amani.

KUNUNUA NA KUSOMA MAGAZETI YA GLOBAL PUBLISHERS ONLINE, INGIA HAPA==>VODACOM M-PAPER APP

*********

JIUNGE NA SOCIAL MEDIA ZETU

KWA HABARI ZA KITAIFA, KIMATAIFA, MASTAA NA MIKASA YA KUSISIMUA

INSTAGRAM: @Globalpublishers

ERIC SHIGONGO INSTAGRAM: @ericshigongo

TWITTER: @GlobalHabari

FACEBOOK: @GlobalPublishers

SUBSCRIBE YOU TUBE: Global TV Online

GLOBAL TV ONLINE: www.globaltvtz.com

HADITHI ZA KUSISIMUA NA MBINU ZA UJASIRIAMALI, ERIC SHIGONGO FACEBOOK PAGE:@shigongotz

Leave A Reply