The House of Favourite Newspapers

Usiku wa Mageuzi ya Bendi… Fm Academia Kulirudisha Sebene Kivingine

0

fm academia-wazee -official imageUwazi Showbiz

WAKONGWE wa Muziki wa Dansi, FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma’ chini ya Prezidaa Nyoshi El Saadat wanatarajiwa kulirudisha sebene kivingine Agosti 12, mwaka huu ndani ya Ukumbi wa Hisaje Park, Boko jijini Dar.

Akizungumza na Uwazi Showbiz prezidaa wa bendi hiyo, Nyoshi El-Saadat alisema kuwa usiku huo utakuwa wa aina yake kutokana na kuwepo kwa burudani mwanzo mwisho.

“Tutatambulisha staili mupya na sebene la aina mupya, niwaombe mashabiki wajitokeze kwa wingi kushuhudia makamuziki ambayo hayajawahi kutokea tangu kuanzishwa kwa bendi hii,” alisema Nyosh.

Mbali na FM Academia, Yamoto Band pia watakuwepo usiku huo ambapo watapiga nyimbo zao zote kali huku wakizindua nyimbo zao mbili, Suu na Mijudo kwa mara ya kwanza ndani ya ukumbi huo.

Binti wa Miaka 19 Aliye Tembea na Wake za Watu Ndiye Huyu Hapa-Part I

PT 2- Binti wa Miaka 19 Aliye Tembea na Wake za Watu Ndiye Huyu Hapa-Part I

Mzungu Dar Afumwa Live Akilawitiwa na Vijana 3, O.F.M Yanyaka Tukio Zima

Leave A Reply