The House of Favourite Newspapers

Waangua kilio mbele ya mkuu wa mkoa

0

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Felix NtibendaARUSHA: Wafanyakazi wa Kampuni ya Sheil Engineering ya Korea inayotengeneza barabara ya njia nne ya Sakina na Tengeru wamejikuta wakiangua kilio mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Felix Ntibenda wakidai kuwa wana kero kubwa ya kunyanyaswa na viongozi wa kampuni hiyo.

Wafanyakazi hao waliangua kilio baada ya mkuu huyo wa mkoa kufanya ziara ya kushitukiza kukagua barabara kwa lengo la kuangalia maendeleo yake wiki iliyopita.

Mara baada ya mkuu wa mkoa huyo kufika eneo la mradi, walimueleza wamekuwa wakitumikishwa bila kuwa na mikataba ya ajira na wamekuwa wakifanya kazi kwa zaidi ya saa 14 kwa siku bila kulipwa muda wa ziada, badala yake wanalipwa shilingi 10,000 tu na wanapodai haki zao, wanafukuzwa kazi.

Mfanyakazi mmoja aliyejitambulisha kwa jina moja tu la Daniel alisema Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa alipotembelea mradi huo hivi karibuni, walimueleza kero hiyo. “Waziri Mbarawa alitoa mwezi mmoja kwa mkandarasi huyo kutoa mikataba ya ajira kwa wafanyakazi wote 400 lakini mpaka sasa hakuna utekelezaji uliofanyika,” alilalamika Daniel.

Akijibu tuhuma hizo, Msimamizi wa Mradi wa Kampuni, Mhandisi Mbaraka Shafii alisema kampuni yao imeshatoa mikataba kwa baadhi ya wafanyakazi na kwamba mchakato huo bado unaendelea ili wafanyakazi wote wapate mikataba yao kama Waziri Mbarawa alivyoagiza.

Akizungumzia kero hiyo, mkuu wa mkoa huo, Ntibenda alimtaka mkandarasi huyo kutoa mikataba ya kazi kwa wafanyakazi wote mara moja na aache kuwatumikisha muda wa ziada bila kuwalipa stahiki zao.

“Pia hakikisheni barabara hii inajengwa kwa kiwango kinachotakiwa na msipofanya hivyo, kampuni hii itachukuliwa hatua za kisheria mara moja,” alionya Ntibenda.

Barabara ya Sakina–Tengeru yenye urefu wa kilomita 14 inajengwa kwa msaada wa Benki ya Maendeleo ya Afrika na inatakiwa iwe imekamilika na kukabidhiwa kwa serikali ifikapo Mei mwakani.

Binti wa Miaka 19 Aliye Tembea na Wake za Watu Ndiye Huyu Hapa-Part I

PT 2- Binti wa Miaka 19 Aliye Tembea na Wake za Watu Ndiye Huyu Hapa-Part I

Mzungu Dar Afumwa Live Akilawitiwa na Vijana 3, O.F.M Yanyaka Tukio Zima

Leave A Reply