The House of Favourite Newspapers

Usiku wa Nishike… Bella, Man Fongo Ndani ya Dar Live

0

BELLAChristian Bella ‘Obama’

Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

KING of the Best Melodies, Christian Bella ‘Obama’ akiwa sambamba na mkali wa Singeli, Amani Hamisi ‘Man Fongo’ wanatarajiwa kuangusha bonge la shoo Septemba 3, mwaka huu ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem jijini Dar.

Man Fongo 'Mzee wa hauna' (2)Akizungumza na Championi Jumamosi, mratibu wa shoo hiyo inayotambulika kama Usiku wa Nishike, Hartman Mbilinyi alisema, usiku huo mbali na Bella na Man Fongo pia burudani itaporomoshwa na mkali anayesumbua kunako Muziki wa Bongo Fleva, Rucky Baby.

“Utakuwa ni usiku wa wakali kutokana na shoo kabambe tuliyowaandalia. Kwa kiingilio cha Sh 10,000 tu utapata kuwashuhudia Kibao Msambwanda wakikata mauno live bila chenga, Bella akiporomosha ngoma zake zote kali ikiwa na hii mpya ya Nishike bila kusahau Man Fongo atawapagawisha na Hainaga Ushemeji,” alisema Hartman.

Leave A Reply