The House of Favourite Newspapers

H Baba: Udalali wa Magari Unalipa Asikwambie Mtu

0

hbabaNicodemus Jonas, Dar es Salaam

SUPASTAA wa Muziki wa Takeu, Hamis Baba ‘H Baba’ ambaye amekuwa kimya kwenye muziki kwa sasa, amefunguka kuwa biashara ya kuuza magari ‘udadali’ ni moja ya miradi inayomuingizia mkwanja wa maana.

Mkali huyo wa ngoma kadhaa kama Poteza, Nibebe na Mpenzi Bubu ameliambia Championi Jumamosi kuwa, sababu za ukimya kwenye tasnia ya muziki kwa muda mrefu kuwa ni kuwa bize na ishu zake zingine nje ya muziki ikiwemo uuzaji magari.

Amesema dili za uuzaji magari amezianza kitambo na ndiyo mradi unaompatia kipato kizuri, lakini akaweka ngumu kulinganisha na kipato anachovuna kwenye muziki.

“Biashara ipo na inaendelea vizuri, ni moja ya biashara inayolipa vizuri lakini siwezi kuanika kwenye vyombo vya habari ninachopata.

“Kweli niko kimya, lakini lazima utambue kimya kina maana kubwa, muda wowote nitarejea kwenye muziki lakini sitaki kuahidi itakuwa lini,” alisema nyota huyo kutoka Jiji la Miamba, Mwanza.

Leave A Reply