The House of Favourite Newspapers

Usipige Bwana…Tuma Meseji!-4

1

ILIPOISHIA GAZETI LA IJUMAA WIKIENDA:

“Talaka umepata mama, tena hakuna kurejeana, Bony naye alimtania Aisha shemejiye huku akimwangalia, walipogongana macho, Aisha aliyakimbiza haraka sana kitendo ambacho Neema alikiona, akakishangaa…

TAMBAA NAYO MWENYEWE…

 

Hata hivyo, Neema alipuuzia akiamini hakuna kitu kibaya katika kuangaliana huko na akajilaumu ni kwa nini amekuwa na mawazo kama hayo kwa mgeni wao!

 “Kuanza kuhisi vibaya mapema yote hii ni kuanza kumpa maisha magumu ndani ya nyumba hii,” alisema moyoni Neema.

Utani ulikatikia hapo, Aisha alikaa wakaanza mazungumzo yenye umakini sasa na kuacha na yale ya mwanzoni ambapo walizungumzia sana maisha kwa ujumla, ugumu, urahisi, maendeleo na jitihada zake.

***

“Darling kama nilivyokugusia muda ule, mimi nilipanga leo chakula cha usiku tukapate mahali penye utulivu, tutoke na Aisha,” alisema Neema…

“Kama ni gharama ni juu yangu,” Neema aliongeza tena.

“Sawa hakuna shida,” alijibu Bony.

Hapo walikuwa chumbani kwao lakini Neema alishamwambia Aisha kuhusu mtoko huo na kigiza kilipoanza alijipara vilivyo ili kutoka.

Bony na Neema walitokea chumbani wakiwa tayari wameshapendeza sana. Walivaa nguo zilizofanana rangi. Walishikana mikono wakati wanatoka nje, Aisha akiwa pembeni ya Neema.

Neema alimtaka Aisha kukaa mbele kwenye gari yeye akae nyuma wakati Bony akiendesha…

“Hapana kaa mbele Neema,” alisema Aisha…

“Noo! Kaa mbele Aisha. Unajua siku zote mke mkubwa anakuwa nyumanyuma, kipaumbele anapewa mke mdogo kwanza maana kipya kinyemi…teh! Teh!” alisema akicheka Neema, Aisha akakaa mbele.

Safari ilianza, mazungumzo yakawa ya kawaida, hasa kuhusu barabara za jiji zinavyoboreshwa. Mazungumzo yao mpaka wakafika kwenye hoteli moja kubwa iliyopo maeneo ya Ubungo, wakakaa hapo.

Walikaa meza moja kwa mpangilio wa Bony kuwa katikati ya Neema na Aisha. Kama mtu angewafuatilia isingekuwa rahisi kujua nani mke wa Bony kati ya hao wawili.

Waliagiza chakula laini na vinywaji pia. Neema aliagizia wine ambayo alisema angeichangia na Aisha huku Bony akinywa ‘ngumu kumeza’.

Iliwachukua lisaa limoja tu, wakaanza kugongana lugha kwa sababu ya pombe au kilevi…

“Mi nikitoka hapa leo narudi kulala kwangu, nimepamisi sana,” alisema Aisha kwa sauti ya ulevi kabisa…

Aaa! Yaani unataka mumeo akisikia aje kumla nyama mume wangu kwa kukuruhusu siyo? Labda kama unataka kwenda kulala kwako leo twende wote, wewe na sisi,” alidakia Neema naye kwa sauti ileile ya kilaji.

“Umeimisi nyumba au umemisi kibaridi cha nyumba?” aliuliza Bony huku akichekacheka…

“Vyote tu,” alisema Aisha huku akiyumba licha ya kwamba alikuwa amekaa.

Kwa sababu ya giza na kulewa, Aisha aliweza kubebanisha miguu yake, akaipandisha kwenye miguu ya Bony na kuchezeachezea.

“Umeanza utani wako mke wangu,” alisema Bony na kumfanya Neema ashindwe kujua ni utani gani aliouanza Aisha lakini baadaye akahisi ni vile Aisha alivyosema vyote tu. Kumbe mwenzake alikuwa anasemea kule kuchezewa miguu.

“Mhudumu,” aliita Neema…

“Naam.”

“Eti choo kiko wapi?”

“Nenda pale panapowaka taa, kata kulia, utakuta mlango, ingia wa mwisho ndiyo choo cha wanawake,” alielekeza mhudumu.

Neema alisimama akatembea kwa kasi kwenda chooni maana alikuwa amevumilia sana.

Huku nyuma, Aisha alimwangalia Bony na kumwambia…

“Unajua uliposema unaanza utani wako Neema angejua kama angejiongeza sana!”

“Hamna, hawezi,” alisema Bony…

“Kweli baby?” alihoji Aisha huku akimsogelea na kutoa ulimi katika urefu wake wote…

“Kweli kabisa baby,” alisema Bony na kuudaka ulimi huo, wakaganda kwa muda huku wakisikika kuhema tu na mihemko ya kimahaba…

“Tusije tukakutwa sweet,” alisema Aisha akitoa ulimi wake huku akiachia tabasamu…

“Tutamwona akitokea kule,” alisema Bony, akaomba tena ulimi, akapewa, wakaganda kwa dakika kama moja, wakaacha.

Neema alitokea huku akilalamikia umbali wa kwenda chooni…

Yaani hawa walitakiwa kuweka Bajaj kabisa, hata kwa mia mia. Ni mbali sana chooni,” alisema Neema akiwa anakaa.

“Do! Ngoja na mimi niende niuone hata huo umbali,” alisema Bony akisimama kwenda chooni…

“Na mimi, ngoja tuongozaje wote shemeji,” alisema Aisha huku akisimama.

Je, nini kiliendelea hapo? Usikose kusoma chombezo hili jipya kwenye Gazeti la Ijumaa Wikienda ijayo.

HADITHI ZA KUSISIMUA NA MBINU ZA UJASIRIAMALI, INGIA NA LIKE PAGE YA FACEBOOK YA ERIC SHIGONGO, BOFYA HAPA ===>https://www.facebook.com/shigongotz/

1 Comment
  1. alex rodrick says

    dahhhh

Leave A Reply