The House of Favourite Newspapers

Usipige Bwana…Tuma Meseji!-9

0

ILIPOISHIA GAZETI LA IJUMAA:

Neema aliamka, akajua mumewe alishatoka chumbani. Akiwa na gauni lake la kulalia, akatoka. Kufika sebuleni hakumkuta mume wake, akaona aende jikoni ambapo aliamini atamkuta Aisha naye atamwambia alipo Bony…

SHUKA NAYO SASA…

 

Ni Mungu tu, ile Bony kumwacha Aisha tu, Neema huyo…

“Jamani mke na mume mnafuatana kama kumbikumbi, bibi mbele, bwana nyuma!” alisema Neema na kumfanya Aisha acheke kicheko cha kinafiki…

“Teh..! Teh..! Teh! Hayo ni mapenzi ya kipwani unaambiwa,” alisema kwa sauti Aisha lakini huku moyoni akisema…

“Ungejua ni kweli na wala si utani ungeanguka ukafa zako. Tena una bahati sana, kidogo utufumanie. Wenyewe tulishazama kwenye mahaba niue.”

Bony alitoka mbio kurudi sebuleni, akakaa huku akihema kwa kasi. Mapigo ya moyo yalikuwa yakimwenda kwa kasi ya ajabu…

“Du! Pale ilikuwa fumanizi laivu…ni Mungu tu! Hivi kwa nini na sisi tulizibana masikio? Ndiyo maana alipokuwa akija hatukisikia akitembea…daa! Ile kali sana…yaani ukisikia ni Mungu tu ndiyo vile,” alisema moyoni Bony huku kinywa kikijaa mate kwa wasiwasi wa kunusurika kwenye fumanizi jikoni.

Neema akaenda kwenye friji ambako alitoa nyama…

“Aisha, mimi naona afadhali tuchemshe nyama tunywe supu! Nyie hali ya jana ya zile pombe mpo sawa kweli? Mimi hapa nasikia kunywa supu tu, tena ya moto sana,” alisema Neema…

“Hata mimi naona,” alisema Aisha.

“Basi tuchemshe kwenye jiko la gesi. Lakini hiyo chai yao we endelea kuiandaa, huenda mume wetu akataka chai, maana huyu naye…”

“Kama ni chai atakunywa mwenyewe sasa,” alisema Aisha.

Supu iliiva, walikunywa wote watatu, baada ya supu, Bony akatangaza kwenda kulala kwa vile bado alihisi uchovu wa pombe za jana yake…

“Jamani, ngojeni nikaupunguze usingizi kidogo,” alisema Bony akisimama…

“Na mimi nakuja,” alisema mkewe, Neema…

“Yaani mimi ndiyo mnaniacha peke yangu siyo kwa sababu wa ubani wangu yupo majuu?” aliuliza Aisha akicheka hali iliyoonesha kuwa, alikuwa akitania tu…

“Wewe ulie, zamu yako si leo,” Neema alimtania pia.

Kweli, baadaye Neema aliingia chumbani kulala sambamba na mume wake akimwacha Aisha sebuleni.

Kutoka moyoni, Aisha alianza kujisikia upweke wa hali ya juu. Aliamini kama mume wake, Mudy angekuwepo na yeye angepumzika naye chumbani kwako…

“Da! Ningejua ningemwambia Mudy aachane na kwenda kusoma, mbona elimu yake ni nzuri tu! Nini kilitokea lakini…halafu yeye kule alikokwenda anaweza kuishi bila mwanamke? Haiwezekani,” aliwaza moyoni Aisha akiwa anabonyezabonyeza rimoti kubadilisha chaneli mbalimbali kwenye televisheni.

Kule chumbani walikokuwa, Neema alianza uchokozi wake kwa mumewe. Mara amshike hapa, mara pale. Mara kule, mara huku, Bony akaanza kuchaji…

“Ina maana hatulali mke wangu? Mbona kama kule sebuleni nilishajieleza kwamba nakuja kupunguza usingizi…” alisema  Bony huku akipiga mwayo wa uchovu…

“Kwani hapa tumekaa mume wangu? Si tumelala wote tena kitandani kwetu,” alijibu Neema huku akimwangalia mume wake kwa kurembua hali iliyomfanya aonekane mrembo zaidi licha ya kwamba alikuwa hajajipodoa…

“Mi najisikia usingizi bwana, tungelala kwanza basi,” alisema Bony…

“Sasa kwani mimi nimekuzuia nini?” alihoji Neema huku akimfinya. Bony alipata akili za harakaharaka kwamba, afadhali aingie kwenye mechi ili kumkata kiu kisha ndipo auchape usingizi wake, hivyo naye alimwanzishia uchokozi wake. Wakachokozana mpaka wakaingia uwanjani.

Sauti za malovee zilimfikia Aisha pale sebuleni, akashtuka. Akatupa rimoti na kusimama kwanza, akasikilizia. Akaanza kutembea kwa kunyata kuelekea kwenye mlango wa chumba hicho cha akina Bony.

Alisimama mlangoni sambamba nao na kusikilizia ambapo aliweza kusikia kila kitu. Hali yake ikawa tete! Alijikuta akijishika mwenyewe, mara kifuani, mara kwenye nido mara ajishike kama vile miss anavyokuwa jukwaani, ilimradi tu alikuwa katika wakati wa mahaba.

Kila hatua ya chumbani alikuwa makini nayo mpaka akashindwa kuvumilia na kukimbilia chumbani kwake, akajitupa kitandani na kuanza kulia machozi kabisa.

Alilia, akalia mpaka macho yakavimba. Lakini mwishowe kuna sauti ilimjia, ikisema…

“Sasa kinachokuliza ni nini? Bony unaye, ukimtaka unampata. Ingekuwa mumeo hayupo na Bony hayupo hapo sawa. Mbona ulishatengeneza mazingira mazuri tu, acha kulia bwana.”

 

Je, unajua kilichofuatia hapo? Usikose kusoma mwendelezo wake katika Gazeti la Ijumaa, siku ya Ijumaa ijayo.

Leave A Reply