The House of Favourite Newspapers

Usiyoyajua Kuhusu Penzi la Blac Chyna & Rob

0
Blac Chyna.

 

MIONGONI mwa matukio yaliyotingisha ulimwengu wa mitandao ya kijamii, ni tukio la hivi karibuni la kufungiwa kwa akaunti ya Instagram ya Robert Arthur Kardashian ‘Rob’, mdogo wa supastaa wa runingani na mwanamitindo, Kim Kardashian, kwa madai ya udhalilishaji uliopitiliza uliofanywa na staa huyo wa Kipindi cha Runinga cha Keeping Up With the Kardashians.

 

Rob alifanya nini kustahili adhabu hiyo kali, ya kuifutilia mbali akaunti yake iliyokuwa na wafuasi milioni 9.9? Stori inaanzia mbali kidogo, takribani mwaka mmoja na ushee hivi nyuma, mchizi huyo alipoangukia kwenye penzi la mwanamke chakaramu, aliyemtesa na kusababisha amwage machozi kama mtoto mdogo, Blac Chyna.

Japokuwa wengi wanamtambua kwa jina la Blac Chyna, jina lake halisi anaitwa Angela Renée White, mwanamitindo na mjasiriamali ambaye kuna kipindi pia amewahi kufanya kazi ya kucheza nusu utupu kwenye klabu za usiku (stripper).

 

Robert Arthur Kardashian ‘Rob’ na Blac Chyna.

 

Wawili hao walipoanzisha uhusiano wa kimapenzi, mwanzoni mwa mwaka 2016, kila mmoja aliwaona kama hawapo ‘serious’. Yaani stripper aanze kudeti na ‘mtoto wa mama?’

Kumbuka hata kimwonekano, wawili hawa wana tofauti kubwa, wakati Blac Chyna akiwa na mwonekano wa ‘demu wa viwanja’, Rob ana mwonekano wa ‘kitipwatipwa’, na muda mwingi anakuwa ‘close’ na dada zake pamoja na mama yake.

Kelele zilikuwa nyingi mitandaoni, wengi wakieleza kwamba Blac Chyna hakuwa akimpenda Rob kama alivyokuwa akimuaminisha, bali alikuwa akitaka kumtumia.

 

Kivipi? Kabla ya kuwa na uhusiano na Rob, Blac Chyna alikuwa akitoka na rapa brazameni, Micheal Ray Stevenson ‘Tyga’!

Ni Tyga ndiye aliyemzalisha Blac Chyna mtoto wa kwanza, King Cairo Stevenson lakini baadaye, penzi lao liliingia shubiri, Tyga akahamishia majeshi kwa Kylie Jenner.

Kama hujui, Kylie ni mdogo wa Rob na Kim Kardashian, yaani ndiye mdogo kuliko wote kwenye familia ya Kardashian na wakati akianza kutoka na Tyga, alikuwa na umri wa miaka 18 tu.

Rob na Blac Chyna wakitokelezea.

Kitendo cha Chyna kutoka na Rob, kilikuwa ni kama kulipa kisasi kwa Kylie, kwamba wewe si umemchukua mpenzi wangu, basi na mimi namchukua kaka yako! Drama zikaanzia hapo.

Mapenzi ya Blac Chyna na Rob, japokuwa yamedumu kwa mwaka mmoja na miezi michache, yalitawaliwa na ‘drama’ za kufa mtu, mara leo wapo pamoja, kesho wamemwagana, mara wanatukanana mitandaoni, mara familia inaingilia kati na kumkataa mwanamke, yaani ilikuwa ni ‘full stress’.

 

Kizuri ni kwamba Rob alifanikiwa kumpa ujauzito Chyna, ambao ndiyo umesababisha kuzaliwa kwa mtoto Dream Renée Kardashian, Novemba 10, 2016.

Mwezi Februari, mwaka huu, wawili hao walimwagana rasmi, mtoto wao akiwa bado mchanga! Kikubwa kilichosababisha wamwagane, ni tuhuma za Rob kwamba kwa kipindi chote cha uhusiano wao, Blac Chyna alikuwa akim-cheat na wanaume wengine kibao!

Akafunguka kwamba amegundua kuwa mwanamke huyo hakuwa akimpenda bali alitaka kumtumia kupata kiki na kulipa kisasi.

 

Yote tisa, kumi ni juzikati Rob aliponasa video na picha za Blac Chyna, akiwa anajiachia na masela wengine kipindi akiwa bado kwenye uhusiano na Rob.

Jamaa akaamua kulipa kisasi na alichokifanya ndicho kilichosababisha Instagram wakaifutilia mbali akaunti yake. Kupitia ukurasa wake, Rob aliposti video inayomuonesha Chyna akiwa kimahaba na mwanaume mwingine.

Akaona haitoshi, akaposti picha

 

Instagram walipoipiga pini akaunti hiyo, akahamia Twitter na kuendelea kuanika maungo nyeti ya Chyna, nao ikabidi waingilie kati na kufuta picha zote chafu na kumpa onyo!

Matukio hayo yakaonesha kumuumiza mno Chyna, kwa hasira naye akaenda mahakamani na mpaka sasa, Rob amezuiwa na mahakama kumkaribia Chyna na mwanaye, kesi ya udhalilishaji nayo inaendelea na akipatwa na hatia, huenda jela ikamhusu! Hayo ndiyo mapenzi ya kiki za pikipiki na visasi ya Blac Chyna na Rob.

Na Hashim Aziz kwa msaada wa mitandao.

Leave A Reply