The House of Favourite Newspapers

Lulu Diva: Sijawahi Kujuta Kumpenda Belle 9

0
Lulu Diva.

MREMBO aliyewahi kutikisa kwenye masuala ya kuuza sura kwenye video za Kibongo, kisha kuhamia kwenye muziki, Lulu Abbas ‘Lulu Diva’ , amefunguka kuwa hajawahi kujutia hata siku moja kuwa na mahaba na mwanamuziki Abednego Damian ingawa malengo yake ya kuwa naye kwenye uhusiano hayakuwahi kufanikiwa.

 

Akizungumza na Uwazi Showbiz, Lulu Diva alisema Belle 9 ni kijana ambaye amewahi kuutesa sana moyo wake na yeye analifahamu hilo kwa sababu alishawahi kumwambia, hata hivyo hakuweza kumkubalia kwa sababu alimwambia kuwa yupo kwenye uhusiano na hakuwa tayari kuchepuka.

Belle 9.

“Sijawahi kujutia kumpenda Belle 9, kwa ndoto za kuwa naye kwa sasa sina tena maana ilishindikana wakati moyo wangu unamhitaji zaidi, kwa sasa nipo kwenye uhusiano, ninampenda mtu niliyenaye lakini hata Belle 9 nitaendelea kumpenda na kumheshimu kwa sababu ni miongoni mwa watu wenye nafasi moyoni mwangu,” alimaliza Lulu Diva.

 

 STORI: BONIPHACE NGUMIJE | UWAZI

Watazame Warembo Wakali Wanaoshiriki Miss Dar Indian Ocean Wakiwa Kambini

Leave A Reply