The House of Favourite Newspapers

UTARATIBU WA KUAGA NA MAZISHI YA MZEE MAJUTO – Video

KUFUATIA kifo cha msanii nguli wa vichekesho nchini, Mzee Amri Athumani aliyeaga dunia jana usiku majira ya saa 2:00 usiku katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam alipokuwa amelazwa akitibiwa, mtoto wa marehemu ametoa ratiba ya kuaga na mazishi ya nguli huyo.

 

Mwili wa Marehemu Mzee Majuto utaswaliwa na kuagwa katika Msikiti ulipo ndani ya Hospitali ya Muhimbili wakati wa Swalat Dhuhr (Swala ya Mchana) leo Agosti 9, 2018 na baadaye utapelekwa katika Viwanja vya Karimjee vilivyopo Posta jijini humo kwa ajili ya waombolezaji wengine na mashabiki zake kupata fursa ya kumuaga.

 

Baada ya Swalat L’laasir (Swala ya Alasiri), majira ya saa 9 mchana mwili wa marehemu Mzee Majuto utasafirishwa kwenda nyumbani kwake Mkoani Tanga ambako maziko yatafanyika kesho Ijumaa baada ya Swalat Dhuhr ( Swala ya Mchana) Tanga Mjini.

 

BREAKING: MAJUTO Kuagwa Karimjee Kuzikwa Tanga!

Comments are closed.