UWOYA AFUNGUKA CHANZO KIFO CHA MBWA WAKE

 

Irene Uwoya

STAA wa filamu Bongo, Irene Uwoya hivi karibuni ameeleza kupata msiba mzito wa kufiwa na mbwa wake aitwaye Kallu ambapo ameongea na Ijumaa Wikienda na kueleza sababu za kifo hicho.  Uwoya alisema mbwa huyo alikuwa akiumwa ugonjwa wa ngozi uliosababishwa na vijidudu flani hivyo kulazimika kumpaka dawa ambayo ilisababisha mauti yake baada ya kuilamba.

“Unajua dawa za kuua vijidudu mwilini kwa wanyama ni kali hivyo Kallu aliilamba, ndiyo ikamuua, imeniuma sana jamani,” alisema Uwoya. Akasisitiza kuwa, baadhi ya watu wanaweza wasielewe ni maumivu ya kiasi gani aliyo nayo moyoni kwa kufiwa na mbwa huyo lakini ukweli ni kwamba amepata pigo.

“Yaani Kallu ameniumiza sana, siwezi kumuelezea mtu akanielewa ila nimeumia mno, itanichukua muda sana kusahau. Alikuwa ni rafiki yangu, nikiwa siko sawa alikuwa akijua, itanichukua muda kukaa sawa,” alisema Uwoya.

Stori: Imelda Mtema,Ijumaa Wikienda


Loading...

Toa comment