The House of Favourite Newspapers

UWOYA Afungukia WEMA Kutembea na Dogo Janjaro

KUFUATIA skendo ya kimapenzi baina ya msanii wa Bongo Fleva, Abdulaziz Chende ‘Dogo Janja’ na staa wa filamu za Kibongo, Wema Isaac Sepetu, mwigizaji wa Bongo Muvi, Irene Uwoya ameifungukia ishu hiyo.

Wakati skendo hiyo inatokea siku kadhaa zilizopita, bado Uwoya alikuwa ni mke wa Dogo Janja kabla ya penzi lao kudaiwa kusambaratika.

 

Katika mahojiano na Risasi Jumamosi, Uwoya alisema kuwa, hakuwa na muda wa kuwauliza chochote kwa sababu wote ni watu wazima.

Uwoya alisema hana mpango wowote wa kuongea chochote kuhusiana na madai hayo kwa sababu kama waliamua kufanya hivyo (kutoka kimapenzi) ina maana hawakuwa vichaa, bali waliamua na walikubaliana hivyo kwa upande wake hawezi kufanya chochote.

“Unajua mimi nipo bize, ninafanya mambo yangu, halafu tena nitenge muda mwingine wa kuwahoji watu wazima wanaojitambua kuwa kwa nini waliamua kutembea na kufanya mapenzi? Kwangu mimi hapana kabisa… sina muda huo, wangekuwa hawana akili nzuri ningesema sawa, lakini ni watu wenye akili timamu kabisa,” alisema Uwoya.

Uwoya alikwenda mbele zaidi na kusema kuwa atashangaa kuona kama Wema atakuwa hajui Dogo Janja alikuwa ni nani kwake (shemeji yake) na yeye Wema ni nani kwake hivyo mtu akijifikiria hawezi kufanya kitu chochote.

 

Alisema katika hali kama hiyo yeye aliishia kuwatazama tu ili aone mwisho wao utakavyokuwa hivyo anashukuru mambo yamekuwa hadharani kwani yeye ndiye alikuwa akionekana mkorofi siku zote.

“Watu wengi wananiona mimi kama ni mkorofi na ndiyo maana niliacha kabisa watu wenyewe wazungumze baada ya kuona vitu vinaendelea, lakini kwa upande wangu  nilinyamaza na sina muda wa kumhoji mtu yeyote.

“Niliamua kuwaangalia tu mpaka mwisho kwani nina vitu vingi vya kufanya ambavyo vinaniumiza sana kichwa changu,” alisema Uwoya.

Hivi karibuni kuliibuka tetesi hizo nzito kupitia mtandao wa kijamii wa Instagram kuwa Wema anatoka kimapenzi na Dogo Janja walipokuwa mkoani Arusha.

 

Wakati ishu hiyo ikishika kasi ndipo Wema alipokumbwa na msala wa kusambaza picha na video chafu kwenye mitandao ya kijamii akiwa na mtu aliyedai kuwa ni mumewe mtarajiwa, Patrick Christopher ‘PCK’ na kusababisha ishu yake hiyo na Dogo Janja kuzimwa.

STORI: Imelda Mtema, Risasi Jumamosi.

MCHUNGAJI MASANJA Afunguka Ishu ya Wema/ Amber Rutty/Pepo la Uzinzi

Comments are closed.