The House of Favourite Newspapers

Watuhumiwa Kumwua Mchumba wa Kaka wa DJ Khaled

Nicole Tuck and DJ Khaled

WATU watano wamefikishwa mahakamani wakidaiwa kumuua Nicole Truck aliyekuwa mchumba wa kaka wa mwanamuziki na prodyuza maarufu wa Marekani, DJ Khaled.

Tukio hilo lilitokea jijini Washington DC ambapo Nicole, mchumba wa Jonathan Tuck (25), aliuawa kimakosa na watu ambao wanaaminika kuwa wezi na walikuwa wanatoroka baada ya kurusha risasi sehemu waliyotoka.

Watu watano wamekamatwa kuhusiana na mauaji hayo na watafikishwa katika mahakama ya shirikisho ya Manhattan; watu hao ni: Richard “Showtime” Jimenez, Kevin “Juice” Cruz, Ira “Malachi” Lawson  na Curtis “Gz” Hines. Mtuhumiwa wa tano ni Luis “PopOff” Semiday, ambaye bado hajakamatwa.

 

Comments are closed.