The House of Favourite Newspapers

Uwoya: Filamu za Bei Rahisi Ni Tatizo!

0
Staa wa Filamu Bongo, Irene Pancras Uwoya.

MASHABIKI wengi wa sinema za Kibongo wanaamini kuwa fani hiyo imekosa ubunifu na mwelekeo, hasa baada ya kifo cha nyota wake, Steven Kanumba ‘The Great’ ambaye alionekana kama mtu mwenye hamu ya kufanya mambo makubwa.

Lakini ifahamike kwamba, hata wakati Kanumba akiwemo, tasnia hiyo ilikuwa na changamoto nyingi, zote zikisababisha kutetereka kwa soko lake na mashabiki wengi kuzikosoa, hasa ukosefu wa uhalisia na waigizaji wengi wa kike kupendelea kuvaa mavazi ya nusu utupu, ambayo yalichangia kwa kiasi kikubwa kuwakwaza mashabiki.

Wakati mashabiki wakiwatupia lawama wasanii kwa kushindwa kuwa wabunifu ili kuendana na mazingira ya jamii, waigizaji nao walikuwa na changamoto kubwa juu ya soko la kazi zao. Katika mahojiano haya, mmoja wa waigizaji wenye majina makubwa wa Bongo Movies, Irene Pancras Uwoya, anafunguka masuala mbalimbali;

Swali: Labda mimi siyo mfuatiliaji sana, lakini naona kama filamu zimesimama hivi au?

Uwoya: Zimesimama unamaanisha nini? Yaani hazizalishwi tena au?

Swali: Ninamaanisha haziko kama ilivyokuwa kipindi cha nyuma, filamu zilikuwa nyingi sokoni na watu wakizigombea, sasa hivi sizioni.

Uwoya: Ni kweli, sasa hivi wasanii wamepunguza kutengeneza kazi mpya, sababu kubwa ni soko, limekuwa gumu sana.

Swali: Limekuwa gumu kivipi?

Uwoya: Hapa pana changamoto nyingi, kwanza kwa wasambazaji wenyewe na pia kwa wanunuzi. Kwa upande wa usambazaji, wananunua kazi kwa bei ambayo inatuumiza na mara nyingi tunakuwa hatuna jinsi, ni bora tufanye kazi tuonekane kuliko kukaa tu nyumbani.

Swali: Huoni kuwa ubora duni wa kazi zenu ulichangia kwa wasambazaji kununua kwa bei ndogo?

Uwoya: Wakati mwingine uduni wa kazi unatokana na haohao wasambazaji ambao wana bei zao.

Leave A Reply