The House of Favourite Newspapers

Uwoya Hana Mizuka Na Mashoga

0
Irene Uwoya.

STAA mwenye makeke kwenye Bongo Movies, Irene Uwoya ameliambia Ijumaa Wikienda kuwa katika maisha yake na miaka yote hajawahi kuwa na tabia ya kubadili marafiki au mashoga na hiyo imemsaidia mno.

 

Uwoya alisema kuwa, marafiki alionao kwa sasa ni walewale wa zaidi ya miaka nane na wala hahitaji kuwaongeza kwani wanamtosheleza kwa kila kitu.

 

“Kitu ambacho kilinishinda mimi jamani ni kubadili marafiki na tabia ya kukaa na marafiki muda mrefu imenisaidia sana kuepukana na vitu vingi mno. Ndiyo maana marafiki zangu ni haohao muda wote na wamekuwa kama ndugu,” alisema Uwoya.

Leave A Reply