The House of Favourite Newspapers

Uwoya: Kama Hutumii Pesa Mtumie Mwenzako “Pesa Huwa Hazitafutwi, Zinategwa…”

0
Staa wa Bongo Movie, Irene Uwoya.

Irene Uwoya; ni bishosti wa Bongo Movies ambaye pesa zimemtembelea.

Uwoya ameendelea kutoa nukuu zinazohusu pesa; awali alisema; “Jumapili siyo siku ya kufua nguo, ni siku ya kutafuta pesa…”

 

Kisha akasema tena; “Pesa huwa hazitafutwi, zinategwa…”

Na safari hii anakuambia; “Usipende kuwa mbinafsi, kama una pesa hutumii, mtumie mwenzako…”

 

Kwa muda mrefu Uwoya amekuwa akisemwa kwamba anatumia vibaya pesa kiasi ambacho atakuja kujutia baadaye na ni bora angetumia pesa hizo kujenga nyumba.

Hata hivyo, Uwoya amekuwa akiwajibu kirahisi tu kwamba, anaishi atakavyo na hakuna wa kumpangia maisha yake aishije.

Stori; Mwandishi Wetu, Dar

Leave A Reply