The House of Favourite Newspapers

Uzi Mpya Yanga Kuzinduliwa Kizungu

YANGA jeuri banaa! Imepanga kuzindua jezi zao za msimu mpya kwenye Hoteli ya Serena ya jijini Dar es Salaam. Wiki hiyo ya Mwananchi yenye kauli mbiu ya Funga Kazi, Kusanya Kijiji kilele chake ni Agosti 4, mwaka huu.

 

Siku hiyo ya kilele, Yanga imepanga kucheza mchezo wake wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Mabingwa wa SportPesa Super Cup, Kariobang Shark’s ya nchini Kenya huku ikitambulisha kikosi chao kipya watakachokitumia kwenye msimu ujao.

Katibu wa tamasha hilo kubwa na kihistoria, Deo Mutta alisema kuwa, kabla ya kwenda kuzitambulisha jezi hizo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam wameandaa utaratibu mpya utakaofanyika Serena Hotel.

 

Mutta alisema kuwa, jezi hizo zitauzwa kisasa kwa maana ya mnada na baadaye kwenda Taifa kutambulishwa kwa wachezaji kuzivaa zote za nyumbani na ugenini.

 

“Tumepanga kutambulisha jezi zetu mpya za msimu ujao tutakazozitumia nyumbani na ugenini kwa njia tofauti katika siku hiyo ya kilele ya Wiki ya Mwananchi. “Siku hiyo kabla ya kwenda kucheza Uwanja wa Taifa kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Kariobang Shark’s tutafanya utambulisho huo Serena Hotel ambako tutaandaa vitu vya utofauti,” alisema Mutta.

Comments are closed.