The House of Favourite Newspapers

Uzinduzi wa JS Hotel…. Abdu Kiba, Ali Kiba, Kuichafua Chato Leo

MKALI wa Bongo Fleva, Abdu Kiba anatarajiwa kufanya bonge moja la shoo katika hafla ya uzinduzi wa Hoteli Mpya ya JS iliyopo Chato mkoani Geita, leo Jumatatu Desemba 25, katika Sikukuu ya Krismasi.

Katik shoo hiyo, Abdu Kiba atapanda jukwaani na mkali Ali Kili ambao kwa pamoja wakitarajiwa kufanya maajabu ya mwaka na kuweka historia katika ardhi ya Chato na vitongoji vyake huku Ali Kiba akitokea kwenye Special Appearance ya jukwaa hilo.

Akizungumza na mtandao wa Global Publishers, DJ Yogo ambaye atasimamia mashine siku hiyo ameeleza kuwa shoo hiyo wameiandaa maalum kwa wakzi wa Chato na viunga vyake kusherehekea vizuri Krismasi kwa kuwapatia burudani ya aina yake.

Ufunguzi wa JS Hotel, Desemba 25 utaanza na sherehe za ufunguzi kuanzia saa 8:00 mchana na kuanzia saa 12:00 burudani za kufa mtu zitagongwa ndani ya Ukumbi wa mpya wa JS Hotel huku kiingilio kikiwa VIP 50,000 na kawaida 10,000.

Leo Desemba 25, Chato patachafuka.

Comments are closed.