The House of Favourite Newspapers

Uzuri wa uwanja usafishwe

PAAAMBE SHOGA… wanakwambia mfuniko wa soda hautunzwi na ukitaka kujua kanga ina umuhimu nenda ukweni na taiti, upo nyonyo? Heee heeeeeiyaaaaa heri uwe na guu la bia kuliko kiuno cha tembo, hujulikani mbele wapi nyuma wapi, shuuutuuuuu!

Usinione nina furaha ukasema leo Anti Naa amelikamatia danga la Kizungu, unikome kama ya Alikiba! Jicho hilo kama kunguru wa Pemba hujulikani unanitazama au unaringa, unaloooooo eeeeh!

Shoga acha niende kwenye kile kinachonikutanisha na wewe kila siku maana ukisikia maneno ya watu unaweza kupasuka kama puto la mtoto anayesherehekea siku ya kuzaliwa. Hivi jamani hadi leo kuna watu hawajui kabisa ubaya wa kufuga kichaka na mtu huyo anajiita anajua mapenzi, shuuutuuuu!

Jitu zima halijui usafi wake zaidi ya kujua ule wa kuchukua ufagio na kuingia uwanjani jamaaaani! Unakuta mwanamke mtu mzima uwanja una nyasi ngumu kama kamba ya katani, uwanja hauna msisimko! Hivi niwaeleze mara ngapi mjue kuwa kijiko ni kijiko hakiwezi kuwa uma?

Mwanamke sharti ujue kuangalia uwanja wako mara kwa mara, sharti ujue siku za kusafisha tena siku hizi wengi wanapenda kusafishiwa na mpenzi, anakaa huku wee unakaa kule basi mnasafishana, rahaaa eeeeh! Pambeeeeeee eeeeh!

Siyo umekazana, unachojua kupaka rangi kucha tena kwa kila staili, msitu umekujaa huko ndani siafu ni wewe, wanyama wa kila aina wanakatiza, kiwanja hata Simba na Yanga hawawezi kuchezea humo hadi unajiuliza huyu anawafugia ng’ombe au kuku?

Shoga ninachoweza kukwambia mwanamke wewe badilika, hata kama mzee naye ana tabia za kufuga uwanja kama anafuga wanyama, mwambie naye abadilike. Siyo wewe unafuga na yeye anafuga, mbaya zaidi mnatoka jasho kama yai viza halafu mnataka kutafuta mtoto, heee heeeiyaaaa!

Kwa leo nisiwe muongeaji sana, kama una akili ya kujiongeza utayafanyia kazi haya yangu na natumai utabadilika shoga yangu! Naomba niishie hapa, ni mimi Shangingi Mstaafu ukipenda waweza kuniita Anti Nasra au Anti Naaa wa Ukwee!

Comments are closed.