The House of Favourite Newspapers

Van Gaal Atumbuliwa Man U

0

van gaal

KOCHA wa Kilabu ya Manchester United Louis van Gaal ametimuliwa rasmi klabuni hapo leo huku aliyekuwa mkufunzi wa Chelsea Jose Mourinho akitarajiwa kuchukua nafasi yake kuinioa timu hiyo.

Mholanzi huyo anaondoka baada ya kukamilisha miaka miwili ya kandarasi yake kati ya huku ukisalia mwaka mmojakukamilisha mkataba wake wa miaka mitatu aliokuwa ameusani Man U.

Ushindi wa United wa Kombe la FA dhidi ya Crystal Palace, mechi iliyopigwa Jumamosi ndiyo ilikuwa mechi yake ya mwisho akiwa mkufunzi klabuni hapo.

Uteuzi wa Mourinho unatarajiwa kuthibitishwa baada ya raia huyo wa Ureno mwenye umri wa miaka 53 kukutana na maafisa wakuu wa United kesho ya Jumanne.

Leave A Reply