Vanessa Mdee Alalamika Kuchafuliwa na Afande Sele
Muda mfupi baada ya msanii wa kitambo kwenye muziki wa kizazi kipya Bongo, Afande Sele kusikika kwenye kituo kimoja cha redio akitoa maneno ya kuudhi kwa wasanii Vanessa Mdee ‘Vee Money’ na Man Fongo, mwanadada huyo ameshindwa kuvumilia na kujibu mapigo kwa mafumbo.
Katika intavyuu hiyo, Afande Sele anasikika akimnanga Vanessa kwamba muziki wake anakopi sana kutoka Marekani, kuanzia sauti, mashairi, mavazi mpaka video, na kusema hawezi kuwa wa kimataifa kama ‘media’ zinavyomnadi, ukimlinganisha na mwanamama Saida Karoli ambaye muziki wake ulikuwa na vionjo vya Kitanzania.
Kupitia Twitter, Vanessa ambaye anafanya vizuri na wimbo wa ‘Duasi’ alioshirikishwa na Legendary Beatz akaandika ujumbe ambao japo hakuandika amemlenga nani, moja kwa moja ulionesha kuwa ni majibu ya kile kilichosemwa na Afande Sele. Tazama alichokiandika: