The House of Favourite Newspapers

Vanessa Mdee: Kuhudhuria Misiba Siyo Matangazo

MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Vanessa Mdee, amejibu tuhuma za kutoonekana misibani hivi karibuni, baada ya kudai kuwa amechoshwa na tuhuma hizo zisiszo na msingi. Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Vanessa amejibu tuhuma hizo na kudai kuwa amekuwa akihudhuria lakini kimya kimya kwani misiba na mazishi ni ibada na hakuna umuhimu kujionesha.

 

“Niliona nipotezee lakini naomba niseme once and for all. Misiba na mazishi ni kama ibada, ukishiriki sio habari ya kutangaza kama tamasha. Nimeona watu wanataka kunishikilia bango kama mtu asiyehudhuria au asiyeshiriki katika ibada hizi.

“Kama unataka kufahamu nilikuwepo katika misiba yote ya hivi karibuni lakini sikupenda kutangaza uwepo wangu kutokana na kupitia misiba mizito katika maisha yangu kama watu wengine wengi.

 

“Siku ya kesho itakuwa miaka 12 tangu nimpoteze baba yangu mzazi na mwaka huu ni miaka miwili tangu nimpoteze Dada yangu ( mtoto wa kwanza wa baba) i bet you didn’t even know, why? Because I prefer to silently pray for the family and loved ones, I’ve found that only God can bring some relief in these situations. “ameeleza Vanessa Mdee na kufafanua.

“Mtu akifiwa anapitia mambo mengi na anahitaji faraja. Nadhani nimeeleweka. Asanteni na Mungu awatunze wote na familia zenu.“

 

Itakumbukwa kuwa Tanzania imekumbwa na misiba ya watu maarufu kwenye tasnia ya habari na burudani kwa wiki tatu mfululizo ikiwemo msiba wa Rapper Godzilla, Mtangazaji wa clouds FM, Ephraem Kibonde na Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba.

Comments are closed.