VAR Yasababisha Balaa Brazil

Chama cha Soka nchini Brazil kimesema kitachukua hatua kali kwa Klabu ya Gremio kufuatia vurugu zilizozuka kwenye mchezo wa Ligi Kuu nchini humo siku ya Jumapili, Oktoba 31, 2021.

.

Mashabiki wa Gremio walivamia uwanja na kufanya vurugu kufuatia kipigo cha 3-1 nyumbani dhidi ya Palmeiras.

Mashabiki hao walijaribu kuharibu Mfumo wa VAR uliotumika kulikataa bao lililofungwa ambalo lingefanya ubao kusomeka 2-2 kabla ya kuongezwa bao la 3.

Matokeo hayo ya kipigo yameifanya klabu hiyo kusalia katika eneo la timu zitakazoporomoka daraja kwenye msimamo wa ligi kuu nchini Brazil.


Toa comment