The House of Favourite Newspapers

Pointi 5 tu, Simba bingwa

KOCHA wa Simba, Pierre Lechan­tre amesema kuwa wanahitaji kupambana kufa na kupona ili ku­fanikiwa kupata pointi tano zitaka­zowawezesha kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara.

Simba inaongoza ligi ikiwa na pointi 62, imebakiwa na mechi nne lakini ikipata poin­ti tano itafikisha pointi 67, Yanga ni ya tatu ikiwa na pointi 48 na hata ikishinda mechi zake sita zilizobaki itafikisha pointi 66.

 

Misimu minne mfululizo Simba haiku­weza kutwaa ubingwa wa ligi hiyo na sasa inaonekana kuwa katika nafasi ya kubeba ubingwa.

Simba imebakiza mechi nne kumaliza mzunguuko wa ligi ambapo inahitaji pointi tano tu ili kuweza kujihakikishia kutwaa ubingwa msimu huu.

 

Akizungumza na Championi Jumatano, Lechantre alisema ; “Nawaandaa wachezaji wangu kwa kuwashawishi wafanye vizuri katika mechi zilizobaki, tunahitaji pointi tano zitakazotusaidia kupata ubingwa, mechi zilizobakia ni ngumu.”

Simba imebakiza mechi dhidi ya Ndanda FC, Singida United, Majimaji na Kagera Sugar ili kumaliza ligi. Lakini Yanga ak­ipoteza mchezo mmoja tu kwa sasa Simba itakuwa tayari bingwa.

Khadija Mngwai, Dar es Salaam

Comments are closed.