The House of Favourite Newspapers

Vee Money, Ruby Waitwa Uzinduzi Women

Ruby

MWANAMUZIKI anayefanya vizuri katika Bongo Fleva kwa sasa, Vanessa Mdee maarufu kama Vee Money na chipukizi Ruby, wameitwa kushiriki uzinduzi wa albamu ya saba ya mkongwe Lady Jaydee iitwayo Woman.

Akiteta na Risasi Vibes juzi, mkongwe huyo alisema ni albamu ambayo angependa uwepo wa wasanii wenzake wa kike na hasa kama angewapata wawili hao pamoja na Shaa, kwani anataka kuona nguvu ya mwanamke inasimama wakati wa uzinduzi huo.

Vee Money (kulia) na Shabiki yake

“Ni uzinduzi ambao nitapiga karibu nyimbo zangu zote hit kuanzia albamu ya kwanza, kwa hiyo utaona ninahitaji muda mwingi zaidi, lakini nitawaalika hao wasanii kama watakuwa na nafasi ili nao waimbe pamoja nami, sifikirii sana kualika wasanii wanaume, lakini wakipatikana poa tu, nitashukuru,” alisema

Comments are closed.