Anajua Aisee! Alichokifanya Joel Lwaga Utafurahi Mwenyewe – Video

JAMAA anajua aisee! Hivi ndivyo unavyoweza kusema kutokana na umahiri wake wa kucheza na jukwaa na kuteka hisia za wasikilizaji au mashabiki wa nyimbo zake hasa anapokuwa jukwaani akitumbuiza.

Mwimbaji wa nyimbo za Injili, Joel Lwaga, amewaacha midomo wazi mashabiki zake baada ya kufanya shoo kwenye kongamano la linalowakutanisha wanafunzi wa vyuo mbalimbali nchini, Victory Campus Night la mwaka 2019, limefanyika katika Viwanja vya Tanganyika Packers jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na umati mkubwa.

Joel ambaye alikuwa mwimbaji mkubwa wa mwisho kupanda jukwaani kwenye kongamano hilo, amewateka mashabiki na kujikuta wakiimba nyimbo zake zote alizokuwa aki-perform wakati wa shoo hiyo bila kujali ni wimbo wa zamani au mpya.

Tamasha hilo lililoandaliwa na Kanisa la VCCT – Mbezi Beach, chini ya mchungaji Dkt. Huruma Nkone, limetikisa Jiji la Dar es Salaam licha ya mvua kunyesha lakini watu walijaa uwanjani na ratiba ikaenda kama ilivyokuwa imepangwa.

 

Katika tamasha hilo, ambalo limeanza majira ya saa 1:00 jioni, waimbaji mbalimbali wamepanda jukwaani kuimba wakimsifu Mungu,  baadhi yao ni Upendo Nkone, Miriam Lukindo Mauki, Joel Lwaga, Kwaya ya Uinjilisti ya Kijitonyama, Ipyana Kibona, Mkhululi Bhebhe kutoka nchini Afrika Kusini na wengine wengi.

 

PICHA NA RICHARD BUKOS | GLOBAL PUBLISHERS

MSIKIE JOEL AKIFANYA YAKE

Loading...

Toa comment