Kartra

Video: Aishi Manula Alivyokimbizwa Hospitali Baada Ya Kupata Majeraha

KIPA wa Simba, Aishi Manula Februari 1, 2021 amepakizwa kwenye gari la wagonjwa baada ya kuumia dakika ya 71 ya mchezo wa Ligi Kuu Bara kati ya Msimbazi na JKT Tanzania unaopigwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

 

Manula alidondoka chini baada ya kuruka pamoja na mchezaji wa JKT Tanzania, kisha Erasto Nyoni alikimbia haraka kumuona na akawaita madaktari.

 

Hata hivyo baada ya madaktari kumpa huduma ya kwanza Manula alionekana hali yake mbaya wachezaji wenzake wakaonyesha ishara ya kumfanyia mabadiliko.

Badae akapakwizwa kwenye gari la wagonjwa na kupelekwa hospitalini.


Toa comment